RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

19.02.2017: WATU WALIOAMUA KUOKOKA SIKU YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B”

Siku ya Jumapili 19.02.2017 watu wengi sana waliweza kuokoka na kumpokea BWANA kuwa Mwokozi wa maisha yao. Mch. Mama Mgetha aliweza kuongoza sala ya toba na kuwaombea. Watu wengi waliweza kufunguliwa na wengine kutokwa na nguvu za giza, mapepo na majini ambayo yalikuwa yakiwatesa kwa muda mrefu sana. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kupita kwa mtu mmoja mmoja na kuwawekea mikono ya Baraka na kuwaombea. Baada ya kuombewa waliweza kubatizwa kwa maji mengi na siku ya Jumanne walianza masomo ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Kama watu tuliokoka tunahitaji sasa kuwaombea hawa ndugu zetu wa kiroho ili wazidi kuimarika kiimani.


Wewe ambaye hukubahatika kufika katika ibada hii ya KUONDOKA KWENYE UTUMWA tunakualika katika ibada ya Jumapili hii itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” au utasikia watu wakisema “Kanisani kwa mama Rwakatare”. Mungu na akubariki sana.