MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

26.02.2017: MCH. NOAH LUKUMAY AFANYA MAOMBI Y KUFUNGUA MILANGO YA MAFANIKIO SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Watu wengi sana milango yao ya mafanikio na afya zao imefungwa na bado hawajitambui. Watu wengi wanateseka na umaskini, vifo na shida mbalimbali kutokana na kufungiwa milango yao ya baraka na mafanikio, Na hii inatokana na watu kuwa mbali na Mungu, kuwa mbali na ulinzi wa Mungu, kuwa mbali na uwepo ya wa Mungu, kuwa mbali na Nguvu za Mungu. Shetani hutumia njia hiyo ya watu kuwa mbali na Mungu na kuweza kuingia katika maisha yao. Na wengine wapo karibu na Mungu lakini kuna kampenyo fulani kameachiwa na shetani anatumia kampenyo hako kupenya na  kuingia katika maisha ya watu na kuanza kuharibu malengo ya watu kwa kupandikiza magonjwa na roho chafu ndani yao.

Mch. Noah Lukumay siku ya Jumapili 26.02.2017 aliweza kukemea hizo roho chafu na kumuomba Mungu aweze kufungua milango ya mafanikio na baraka kwa watu. Watu wengi sana walilipuka mapepo na kukimbilia madhabahuni wakihitaji kukombolewa kupitia damu ya Yesu Kristo. Hakika Mungu alikuwa mwema sana kwani walio wengi waliokombolewa na sasa milango yao ya mafanikio iko wazi kupitisha baraka zao kutoka kwa Mungu Baba.

Yawezekana na wewe unapitia majaribu mbalimbali na huoni mpenyo. Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa utasikia watu wakisema kanisani kwa mama Rwakatare, ingia humo na baada ya ibada utarudishwa kituoni. Ubarikiwe na Bwana.

Mch. Noah Lukumay
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare