RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAKONDA ATAJA MAJINA MENGINE 65 YA WATUHUMIWA WA KUUZA ‘UNGA’, WAMO MBOWE, MANJI, IDD AZZAN NA GWAJIMA

 

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaja majina ya watuhumiwa wengine 65 wa madawa ya kulevya, wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Elikael Mbowe, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Askofu Josephat Gwajima na Mbunge Mstaafu wa Kinondoni, Idd Azzan.

Makonda amesema hii ni awamu ya pili ya oparesheni ya kusaka watuhumiwa wa mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya, ambapo amesema awamu hii itakuwa ngumu ikilinganishwa na ile ya kwanza iliyohusisha polisi na wasanii kukamatwa.

Makonda amewataka watu wote 65 waliotajwa, kuhakikisha wanaripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Sentro) siku ya Ijumaa saa 5 asubuhi kwa mahojiano zaidi.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Makonda amesema kuwa, waliokamatwa awali ndiyo waliofanikisha kupatikana kwa orodha hiyo mpya.

Makonda amesema haya.

“Leo tunaingia awamu ya pili ya kampeni ya kutokomeza baiashara haramu ya madawa ya kulevya, kampeni hii ambayo inahitaji watu wenye hofu ya mungu. Niwaombe tuungane sote kumuunga Mkono Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli ili kutokomeza bishara hii.

“Watu wanachanganya, kuna tofauti kubwa kati ya kuitwa na kukamata, unapoitwa na mkuu wa mkoa unapewa haki yako ya msingi ya kusikilizwa, kwa hiyo hawa watu wajitokeze waje tutasikiliza maelezo yao. Kati ya hao 65, kuna wengine ni wauzaji wa madawa, wengine wamiliki wa kumbi za starehe ambazo ndani yake biashara hii inafanyika na wengine wanaufahamu vizuri huu mtandao hivyo watatupa ushirikiano ili kuwakamata wahusika.

“Kampeni ya madawa ya kulevya siyo ya kufanya kimya kimya, tunataka hata mtoto wa shule ya msingi aelewe kama madawa ya kulevya ni hatari. Alisema Makonda.