RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MJADALA WAZUKA KUHUSU AFYA YA KIAKILI YA TRUMP


Ni suala ambalo hungetarajia watu walizungumzie hasa kuhusu mtu ambaye amekuwa akisimamia biashara ya thamani ya mabilioni ya dola na alishinda mpinzani wake Hillary Clinton katika uchaguzi mkuu uliokuwa na ushindani mkubwa mwaka jana.

Lakini sasa wataalamu wa afya ya kiakili wanajadili hali ya rais wa Marekani Donald Trump.

Mjadala huo umekuwa wazi sasa baada ya wataalamu kadha kuandika barua ya wazi wakisema Trump ana matatizo makubwa ya kiakili na hafai kuwa rais.

Wito huo unaonekana kwenda kinyume na msimamo wa muda mrefu wa wataalamu wa kutojadili matokeo ya uchunguzi kuhusu afya hadharani.

Barua hiyo imeshutumiwa na baadhi ya wataalamu.
Mmoja amesema ni ya aibu na sawa na matusi kwa wagonjwa wa matatizo ya kiakili.

Mjadala unahusu nini?
Mjadala kuhusu afya ya kiakili ya Bw Trump si jambo geni, na ulikuwepo hata kabla ya kuchaguliwa kwake kuwa rais Novemba wmaka jana.

Lakini wataalamu wengi wa afya ya kiakili wamejizuia kutoa taarifa hadharani, kutokana na kanuni ya wataalamu hiyo ifahamikayo kama "Goldwater rule", ambayo iliidhinishwa na Chama cha Wataalamu wa Masuala ya Kiakili Marekani (APA) mwaka 1973.

Kanuni hiyo huwazuia wataalamu kujadili matokeo ya uchunguzi na mtu ambaye hajachunguzwa yeye binafsi.

Ilichapishwa kwenye jarida baada ya maelfu ya wataalamu mwaka 1964 kuanza kuuliza maswali kuhusu iwapo mgombea wa chama cha Republican Barry Goldwater alifaa sawa kiakili kuruhusiwa kuwa rais.

APA walitahadharisha mwaka jana kwamba kuvunja kanuni hiyo katika kujaribu kuwatathmini wagombea wa urais lingekuwa jambo la "kutowajibika, lenye uwezekano wa kudhalilisha, na bila shaka ni kinyume na maadili".Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionTrump alikuwa akishindana na Hillary Clinton wa chama cha Democratic

Lakini sasa, baadhi ya wataalamu wameamua kuzungumza hadharani, wakiwemo kadha ambao wametia saini ombi la kutaka Trump aondolewe madarakani.

Ombi hilo kufikia sasa limeidhinishwa na watu 23,000.
Baadhi wanasema huenda Bw Trump ana tatizo ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Narcissistic Personality Disorder (NPD).

Watu wenye tatizo hilo, kwa mujibu wa Psychology Today, mara nyingi huonesha dalili zifuatazo:
Majivuno, kutowahurumia watu wengine na kutaka sana kutukuzwa na kusifiwa.
Huamini kwamba ni wakuu kuliko watu wengine au kutaka kushughulikiwa tofauti na wengine/kupendelewa
Hutafuta sana kusifiwa na kuangaziwa na watu, na hutatizika sana kukubali ukosoaji au kukubali kushindwa.

Kuna jipya?
Kwenye barua waliyoituma kwa New York Times, wataalamu hao 35 wametahadharisha kwamba "udhaifu mkubwa wa kiakili" unaodhihirishwa kwenye hotuba na vitendo vya Trump unamfanya "kutoweza kuhudumu vyema kama rais".

Walisema walikuwa kimya kutokana na kanuni ya Goldwater, lakini sasa wakati umefika kwao kuzungumza.

"Kimya chetu kimesababisha kushinda kwetu kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wanahabari na wabunge wa Congress waliojawa na wasiwasi. Tunahisi kwamba mambo yamezindu na hatuwezi kunyamaza tena."Haki miliki ya pichaAP

Kwenye barua hiyo, wanasema katika hotuba na vitendo vyake, Trump ameonesha kwamba hawezi kuvumilia misimamo ya watu wengine.

Aidha, huwakaripia watu.

"Maneno na vitendo vyake vinaashiria mtu asiyeweza kujiweka katika nafasi ya watu wengine," wanasema.

"Watu wenye tatizo hili hubadilisha uhalisia kujifaa, hupinga na kushambulia mambo ya kweli na wale wanaowapa habari za kweli (wanahabari na wanasayansi)".

Mapema wiki hii, seneta wa Democratic Al Franken alisema wenzake "kadha" kutoka chama cha Republican wameeleza pia wasiwasi kuhusu hali ya kiakili ya Trump.