MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

NI AFRIKA KUSINI TENA-MUHUBIRI AWANYWESHA SUMU YA PANYA WAUMINI ILI KUWAPIMA IMANI


Muhubiri mmoja anayefahamika kama Mtume Light Monyeki nchini Afrika Kusini amewapa waumini wake maji aliyo yachanganya na sumu ya panya kwenye dumu la plastiki.

Baada ya kuyaombea aliwaambia waumini wake hayana madhara tena na kunywa yeye kwanza kabla ya waumini wake na kuwataka wapite mbele kunywa mmoja mmoja.

Aliwambia wanye sumu hiyo kuonyesha imani zao,na wengi walifanya hivyo taarifa kutoka page ya kanisa zilisema.
Light Monyeki,ambaye anaongoza kanisa la Grace Living Hope Ministries mjini Pretorria,anasema kuwa kwa kunywa sumu hiyo,inaonyesha kuwa kifo hakina nguvu kwa waumini.

Picha kwenye ukurasa wake wa Facebook, zinamuonyesha akichanganya dawa inayotumiwa kuua panya kwenye chupa na kuinywa na kisha kuwapa waumini.
Bwana Monyeki ni mhubiri wa hivi majuzi kuripotiwa kuhusika na visa vyenye utata kanisani.