RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

19.03.2017: WATU WAFUNGULIWA KATIKA KIPINDI CHA MAOMBEZI NA UPONYAJI KATIKA IBADA ILIYOFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayofanya katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kupitia mtumishi wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Siku ya Jumapili 19.03.2017 katika kipindi cha maombezi kilichoongozwa na Mch. Noah Lukumay tuliweza kuona uwepo wa Mungu na Nguvu za Mungu zikifanya kazi na kuharibu kazi za shetani. Watu wengi sana waliweza kufunguliwa na kuweka huru baada ya kufanyiwa maombezi. Kwa kipindi kirefu sana watu wamekuwa katika mateso makubwa wakinyanyaswa na shetani lakini baada ya kukanyaga katika madhabahu ya Mlima wa Moto wengi wao walipokea majibu yao. Mungu ni Mungu wa huruma na upendo wala habagui kabila la mtu, rangi ya mtu, dini ya mtu, bali Yeye akiamua kufanya kazi yake hufanya kwa haki.

Yawezejkana na wewe unapitia magumu, umehangaika bila msaada, lakini leo hii umepata bahati ya kusoma ujumbe huu, ninakuomba Jumapili hii usikose kabisa katika ibada itakayoanza saa 3 asubuhi hadi 8 mchana. Yawezekana unatafuta kazi, mchumba, mtoto, kiwanja, nyumba, gari, safari za nje, kibali, kupendwa kazini kwako, amani katika ndoa yako na familia yako, watoto kufaulu mitihani na mambo mengine kama hayo. Usihangaike njoo kwa Yesu na utaona majibu yako. Mungu anakupenda, Mungu anakuhitaji kwa kazi yake. Jumuika na wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" nao watakusaidia kukuongoza katika njia sahihi ya kufika mbinguni kwa Baba. Ubarikiwe na Bwana.


 Mtoto wa Mzee Kandolo akiombewa