23.04.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWATAKA WATU KUWA NA UMONA NA LUGHA MOJA NDANI YA KANISA.
Siku ya Jumapili 23.04.2017 ya KIPOKEA HABARI NJEMA
katika kanisa la Mlima wa Mlima wa Moto
Mikcheni “B”, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alisisitiza kanisa kuwa na
umoja na kuwa na lugha moja, na hivi ndivyo alivyoanza kusema;
Bwana asifiwe sana. Tusome Neno
la Mungu kitabu cha Mwanzo 11:1-9, Biblia inasema, “ Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja ikawa watu
waliposafiri, pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari
wakakaa huko. Wakaambiana, haya na tufanye matofari tukayachome moto. Walikuwa
na matofali badala yam awe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, haya na
tujijengee mji na mnara na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina, ili
tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akashuka ili auoni mji na mnara,
waliokuwa wakiujenga wanadamu. Bwana akasema Tazama watu hawa ni taifa moja na
lugha yao ni moja na haya ndiyo wanayoanza kufanya, wala sasa hawatazuiliwa
neno wanalokusudia kulifanya. Haya na tushuke
huko tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. Basi
Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote, wakaacha kuujenga ule
mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli, maana hapo ndipo Bwana
alipoichafua lugha ya dunia yote, na kutoka huko Bwana akawatawanya, waende
usoni pa nchi yote.”
Nitasema kwa ufupi, lakini
lengo la ujumbe huu ni tuombe kwa ajili ya kanisa letu. “Ninaomba kwa ajili ya
umoja wa kanisa, ninaomba kwa ajili ya mshikamano wa kanisa letu.” Nilipokuwa safari (afrika Kusini) Mungu
alisema na mimi utakaporudi nyumbani,
chukua muda mwingi hata kama ni mwezi mzima kuligusa kanisa, kugusa mioyo ya
kila mmoja waweze kurudi katika upendo ule wa kwanza tulioanza nao.
Ndugu zangu tulipewa amri mpya
katika Yohana 13:34 Yesu kasema, “amri mpya nawapa pendaneni”, anasema
pendaneni mpaka wamataifa wajue kweli ninyi ni wanafunzi wangu. Na kweli ukiingia
katika kanisa la watu wa Mungu kitu cha kwanza kitakachokugusa ni upendo wao
kwa sababu hata kama hakujui atakuuliza, na mimi nilitokea katika dini ya
Romani Katoliki ambako watu wanaposalimiana wanakumbatiana kama ishara ya
upendo. Nilipokuwa Katoliki baadae nikaanza kuelewa kuwa ule ulikuwa ni upendo
wa kweli, waliwatambua wapendwa Wakristo kwa sababu ya kupendana kwao.
Upendo ule wa kwanza urudi
tena nyumbani mwa BWANA, tukitoka nje tusisalimiane tu tunaojuana, tusalimiane
na wageni, wakina mama, wamama, wengine wanakuja kanisani lakini hawana upendo
wa kweli. Kama wewe unakaa kule shuka nenda kamtafute mama mwingine awe rafiki
yako, tusikae wenyewe kwa wenyewe tu, kanisa litaongezeka kama kila mtu
atachukua rafiki nyumbani mwa Bwana. Umoja unamtisha hata Mungu, na umoja ndio
ulioweza kusimamisha falme za Kiarabu, falme za Kiarabu ziliweza kusimama kwa
sababu walikuwa na umoja hawakuweza kumtoa Sadam Husseni kwa sababu walikuwa na
umoja, walikuwa na mshikamano, walimpenda, hawakuweza kumtoa Gadafi kwa sababu
walikuwa na mshikamano, lakini mitandao ilivyokuja, na utandawazi ulivyokuja
vijana wakaanza kutuma message kuwa hawa wazee yaani Sadam na Gadafi tuwatoe madarakani na ndio ukaona falme za Uarabuni zikaanza
kusambaratika.
Umoja unafanya tusimame pamoja, na Yesu kabla
ya kuondoka kitabu cha Mathayo 17 kinasema, akasema, “Nimewaombea hawa wachache ambao wao
wamemwamini Kristo, wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja, umoja ni nguvu ya
kanisa, hapa tunaona wenzetu katika kitabu cha Mwanzo 11, walikuwa
wameshikamana wakiwa na lugha moja nia moja ya kujenga mnara mmoja ili wakamuone
Mungu, wakaanza kujenga, Mungu alivyochungulia akaona mnara karibu unatoboa,
akasema hawa watu tusipoenda kutawanya mbinu zao, hakika wataingia hapo. Na
ndio leo hii unaona kuna lugha tofauti kama vile Kinyakyusa na lugha mbalimbali
ziliingia. Anasema wakashindwa
kusikilizana, kiongozi akisema, leta
tofali huyu analeta panga yaani analeta kitu tohfauti kwasababu hawasikilizani
kutokana na lugha kusambaratishwa, kuanzia hapo kujenga mnara kukaisha hapo wakaamua wakabomoa
mnara wao.
Katika kila ushirika kama
hakuna lugha moja, nia moja hamuwezi kufaulu, lakini mkishikamana mtafanya
makubwa. Sisi ni familia ya Kristo, sisi ni watu wa Mungu ni mfano kwa
wamataifa, tukishikamana tutafanya makubwa, tukishikamana watajua kuwa
tumeokoka, tukishikamana Dar es Salaam itaokoka, tukishikamana kanisa hili
tutalivunja tutajenga kanisa la ghorofa, bila kujari unapesa au hauna pesa,
tukishikamana watu wengi wataongezeka kanisani kwa sababu wataona tumeokoka,
watu wengi wanaangaliaga hawa watu wapoje, wakiona tun watu hawaelewani
wahawezi kuja kanisani lakini wakiona watu tumeshikamana, tuna umoja,
tunatembelea kama hivi tunatembeleana, hapo ndipo unakuta mtu anasema hii
familiya nzuri acha nijiunge nayo kwahiyo ningependa kukuasa hata kwa viongozi,
sisi ndio barua iliyowazi kwa wengine, lazima sisi kwa sisi tushikamane, lazima
sisi wenyewe tupendane, mmeacha historia, mmeacha mtetemeko Dodoma, mmeacha
simulizi Dodoma kwa ajili ya umoja wa kanisa hili viongozi mbalimbali wanakuja
walikuja ili kuungana nasi katika sherehe hii ya furaha ya kuapishwa kwangu huu ni umoja wetu wa
kanisa, wanasema jamani hawa watu ni wa namna gani, wale waliovaa sale nyekundu
wakapiga picha, watu wakasema mama yangu ni nini hiki sijawahi ona, wakina baba
wameva suti zao nyeusi ta tai nyekundu watu wakashangaa kwa sababu ya umoja
nawasihi ndugu zangu mbalimbali, karibuni Mlima wa Moto, kanisa ni safina,
ndani ya safina kuliingia nyoka, ndege, samba, mbwa, kuliingia wanyama wa kila
aina wawili kwa wawili, lakini midomo ilifungwa ya samba asione mbuzi, midomo
ilifungwa asiweze kummeza mbwa, unajua kiasilia mbwa na chatu, kama kuna
kumaku, chatu akiachama mdomo mbwa analia mwenyewe anajipelea anajua anaenda
kumezwa sasa sumaku inamvuta, lakini midomo ya chatu ilifungwa kwa sababu
ilikuwa kwa ajili ya umoja na hapa kanisani kwetu sisi tuwefamiliya moja lazima
tuwe wamoja aliyejuu ashuke ammbebe wa chini tukisaidiana kanisa tutasonga
mbele, tukibebana kanisa litaendelea tuko hapa kwa ajili ya kusaidiana, tuko
hapa kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo, huwezi kumuona Mungu mzimamzima
lakini mimi nitakapo kusaidia ndio Mungu ananitumia kwa mfano wake tu, kwa
hivyo lazima tujishuhulishe katika misingi ya kupendana, kushikamana,
kuchukuliana tofauti zetu tuziache, sisi ni ndugu, sisi ni wamoja, mimi
nikipata na yeye kapata ndio maana tunachukua simu zenu, mkiwa na shida
msikwame tukusaidie ili tukubebe, tukukwamue, mimi ni mama yenu wa kiroho na
mama lazima nijari maisha yako. Mungu anajari umoja, na Mumngu anajali
tunapochukuliana na Mungu anaribariki kanisa ukisoma Matendo 2:41 Nao
waliolipokea neno lake wakabatizw, na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu
tatu. Wakawa wakidumu katika fundishola mitume na katika ushirika na katika
kuumega mkate na katika kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu, ajabu nyingi na
ishara zikafanywa na mitume. Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja na kuwa
na vitu vyote shirika, wakauza mali zao na vitu vyao walivyokuwa navyo na
kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. Na siku zote kwa moyo
mmoja, walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba na kushiriki
chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe. Wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu
wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. Umoja
ukaleta maajabu nyumbani mwa Bwana, Mungu anashuka na anaonekana.
Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare