RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Jiwe kubwa lapita karibu na Dunia



Asteroidi kubwa ambayo inakadiriwa kuwa na ukubwa karibu sawa na wa wa Jiwe la Gibraltar imepita salama karibu an Dunia.

Asteroidi hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na kipenyo cha karibu kilomita moja, ilipita karibu na dunia umbali wa mara tano hivi umbali kati ya Dunia na Mwezi.

Jiwe hilo ambalo limepewa jina 2014 JO25, ndilo kubwa zaidi kupita karibu na dunia tangu 2004.

Wataalamu wa anga za juu walisema fursa nzuri zaidi ya kutazama asteroidi hiyo angani itatokea Jumatano usiku.

Picha za mitambo ya rada zilizopigwa kwa kutumia antena ya Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) iliyo na urefu wa 70m (230 ft) katika kituo chake California zilionesha kwamba jiwe hilo lenye umbo la njugu linazunguka mara moja kila baada ya saa tano.Haki miliki ya pichaEPAImage captionJiwe hilo lilikuwa na ukubwa sawa na wa Gilbratar

Asteroidi hiyo iliipita Dunia katika umbali wa kilomita milioni 1.8 (maili 1.1 milioni) saa 13:24 BST mnamo Jumatano, 19 April.

Inakadiriwa kwamba jiwe jingine kupita karibu na dunia itakuwa mwaka 2027 pale asteroidi ya kipenyo cha karibu mita 800 (nusu maili) iliyopewa jina 1999 AN10 itapita karibu na dunia umbali sawa na wa mwezi kutoka kwa Dunia, takriban 380,000 km (maili 236,000 ).