MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

Kutana na Kijana Anayetafuna Chupa na Misumari

KIJANA mmoja aliyejitambulisha kwa jina la James John mkazi wa Mchikichini jijini Dar es Salaam ameonakana kuwashangaza watu wengi wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya kuwa kivutio kikubwa kwao alipoonekana akitafuna vitu vya ajabu vikiwemo vipande vya chupa na misumari.


Mtandao huu ulipata fursa ya kuzungumza na kijana huyo ambaye alieleza kuwa yeye ni mzaliwa wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kogoma na alikuja jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupanua uwezo wa kipaji chake cha sanaa.


…Akilimeza betri hilo.

Ameeleza kuwa katika sanaa yake anao uwezo mkubwa wa kufanya vitu vya ajabu vinavyoweza kushangaza watu kiasi cha kutokuamini kile anachokifanya. Miongoni mwa matukio yaliyoshuhudiwa na kamera yetu ni kutafuna vipande vya chupa, kulalia kibao chenye misumari bila kumchoma na kutafuna misumari.


James John akiwaonyesha mashuhuda betri la redio kabla ya kulitafuna na Watu wakimshangilia.

Mbali na hayo, kijana huyo ameeleza kuwa pia anayo staili ya kubadilisha mkanda kuwa nyoka na kunywa maji lita 20 papohapo.


Baadhi ya wananchi wakimkagua mdomoni kama kweli amemeza msumari.

Katika kuonyesha shoo yake, hutoza kiasi cha Sh. 100 na kuendelea kulingana na wananchi wanachomchangia.


James akitafuna msumari.