RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAFANIKIO; KABLA HAIJAWA CHAPATI ILIKUWA NGANO

Napenda chapati haswa aliyoipika mama. Nikila na maharage huwa nashiba zaidi. Sijui kama na wewe unapenda chapati.

Leo Nataka tujifunze kitu kutoka kwenye chapati. kabla ya kuwa chapati ilikuwa ngano. Ngano ambayo ukiitazama haivutii inafanana na unga wa mahindi au chokaa laini. Ngano ambayo inaweza kutoa vitafunwa vya namna mbalimbali kama vile maandazi,vitumbua, keki, mikate n.k. Hivyo karibia kila mtu mwanzo huwa kama ngano kabla ya hajaamua awe chapati,mkate,maandazi au keki.

Chapati kabla ya kuwa cha chapati ilikuwa ngano. Ilipoanza kuwa chapati ilikandwa, ilichanganywa na maji ya moto au baridi na mafuta kidogo na mkaandaji anaanza kukunda. Anatumia nguvu nyingi kukanda. Ndivyo ilivyo ukiamua kuwa mtu Fulani lazima ukubali kukandwa, ukubali kuchanganywa na maji ya moto ili ukandike vizuri. Dunia inaweza kukuchanganya na kujiona huvutii au hufai,kumbuka na chapati pia hupitia sura hiyo ya kutokuvutia.

Mara umejifunza hili matokeo yake unafeli wala usikate tama jua ndo kukandwa huko ili uweze kufikia malengo yako.

Ngano inapomalizizwa kukandwa huwekwa kwenye kibao cha kusukumia. Huanza kusukumwa na kuchongwa kuwa kwenye umbo la chapati. Unaweza ukawa unajiona ueshakuwa mwanamziki kumbe bado ndio kwanza unasukumwa kuwa mwanamziki. au kazi ,mfanyabiashara au kazi yeyote ile. Inakubidi utulie na kukubali kutengenezwa. Wala usiwe na haraka kuwa na umbo la chapati hukumaniishi ushakuwa chapati.

Ikishatoka kwa kibao na kuwa na umbo la chapati.Hupelekwa jikoni.huwekwa juu ya kikaango bila kupitia katika changamoto. huwezi kuwa vizuri katika fani au taaluma unayotaka kuwa bila kupitia changamoto tambua ya kuwa changamoto ni sehemu ya mafanikio yako.

Kama vile ambavyo dhahabu ili ing’ae vizuri hupitishwa katika moto ndivyo na wewe ili uwe mwenye manufaa katika jamiilazima upitie changamoto. Chapati isipopitia katika moto wala huwezi kuila maana tumbo laweza uma.Ndivyo hata wewe usipopitia changamoto mafanikio hayawezi kuja.

Ndivyo ulivyo kwa kila mtu unayemuona ni maarufu au aliyetenda makubwa katika sayari hii.Kabla hajawa hivyo alikuwa mtu wa kawaida sababu kabla haijawa chapati ilikuwa ngano. Sasa sio wote tutakuwa chapati, Wengine watakuwa maandazi lakini nayo kuna hatua yamepitia ambayo sio lakini tofauti sana na chapati.

changamoto za kimafanikio hutofautiabna kama ilivo chapati huiwekwi amira maandazi huwekwa amira.Tambua mafanikio bila changamoto hayakamilika.lazima upitie kama yalivo maamdalizi ya chapati. Pia usikate tama kwa kile kinachotokea katika maisha yako bali pambana.