MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MATUNDA AINA 5 YANAYOWEZA KUKUPATIA MUONEKANO MZURI WA NGOZI YA MWILI WAKO


Baadhi ya watu wamekuwa wanachukulia kirahisi ulaji wa matunda, lakini unapaswa kujua kwamba matunda ni muhimu kwa afya zetu kwani yanatukinga na magonjwa mbali mbali na pia hutengeneza muonekano mzuri wa ngozi ya miili yetu.

Kunakila sababu za kukubali kuwa matunda ni muhimu sana kwa afya zetu kwa sababu huongeza vitamin kibao; zifuatazo ni sababu zinazokufanya ule matunda kila siku:

AVOCADO: Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juice, lakini huenda watu wakawa hawalipendi kwasababu ya kutokuwa na sukari katika radha yake. Tunda hili linavitamini kibao, ambapo pia huongeza mafuta mwilini, kwa wale walitumialo mara kwa mara.Unashauriwa kula au kunywa juice ya avocado wakati wowote endapo kama huna matatizo yoyote yanayohusiana na kuzidi kwa mafuta mwilini.Pia tunda hili huongeza uzito endapo utalitumia mara kwa mara.

APPLE: Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamini na madini kibao, pia lina kazi kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri wa ngozi ya mwili wako.Tunda hili husaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kuhifadhi ngozi isipoteze uhalisia wake.

NDIZI: Hili pia ni tunda lenyejina kubwa kwa watu wengi wanaojali ulaji wa matunda, kwani nitamu na lenye ladha safi.Tunda hili husaidia kulainisha ngozi ya uso iliyokauka, kwa mfano utakuta kuna baadhi ya mafuta au losheni zimecholwa ndizi.Kula ndizi ili urekebishe ngozi ya uso wako pamoja na kuupa uwezo mzuri wa ukumeng'enya chakula.

PAPAI: Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai pia hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha utaona kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.

CHUNGWA: Hili ni chungwa maarufu sana linalosaidia kurudishia ngozi iliyodhurika na kuupa uhalisia wa ngozi yako. Jinsi ya kutumia ni rahisi sana, chukua juisi ya chungwa ya baridi kisha paka usoni, acha kwa dakika 10 kisha osha utaona matokeo yake.