VIDEO: Maamuzi ya serikali kuhusu Madaktari 258 waliotakiwa kwenda Kenya


Rais wa Tanzania ameamua madaktari wote 258 waliokuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na Serikali ya Tanzania mara moja.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Ummy Mwalimu amesema Rais Magufuli amefikia uamuzi huo kutokana na utayari waliouonesha madaktari hao pamoja na wataalamu wengine 11 lakini kwa kuwa kuna pingamizi lililowekwa huko Kenya basi Serikali ya Tanzania itawaajiri wote.