RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

14.05.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWAOMBEA WACHUMBA WALIOVISHANA PETE SIKU YA MOTHER'S DAY MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili ya Mother's Day tarehe 14.05.2017 ilikuwa ni siku ya baraka kwa wapendanao hawa ambao walionyesha msimamo wao wa uchumba baada ya zoezi zima la kuvishwa pete ya uchumba kufanyika. Zoezi hili lilifanyika katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" likiambatana na maombezi kutoka kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare pamoja na kanisa zima la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Mungu wetu tunayemuabudu na kumwamini, mara nyingi hutenda mambo yake kwa ukubwa kwa walio wake. Miujiza Yake yashangaza walio wengi katika kanisa hili.

Wapo watu wengi wanatamani kuoa/kuolewa lakini milango yao imefungwa na maadui zao. Kila wakichukua hatua ya kufanya uamuzi wa kuoa au kuolewa, vikwazo vinajitokeza. Wengine wanakumbwa na tatizo la fedha, wengine hawapati yule wanaompenda, wengine ni kutokana na makabila yao kutompenda mke/mume, wengine ni roho chafu zilizomo ndani yao zinazuia kuoa/kuolewa, wengine ni majini mahaba n.k. Lakini nataka kukuambia kuwa huyu Mungu tunayemwabudu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ni Mungu wa majibu. Tumeshuhudia ndoa nyingi zikifungwa mahali hapa na hii ni kwasababu ya ile neema ya BWANA ambayo ameachilia katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Yawezekana unatamani sana kuoa au kuolewa, na umehangaika sana bila kupata yule wa kuoa au kuolewa naye. Ushauri wangu ni wewe kujitahidi sana kuhudhuria ibada za mahali hapa na utaona mkono wa Mungu ukifunguka juu yako. Jitahidi kuyafanya yale mapenzi ya Mungu unayofundishwa na watumishi wa Mungu, soma sana Neno la Mungu, jitakase, onyesa upendo kwa kila mtu, uwe mtoaji, ungama dhambi zako kila wakati, saidia wenye uhitaji wa kusaidiwa, fanya yaliyo mema kwa kila mtu.

Ibada zetu siku ya Jumapili zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ni saa 9 mchana hadi saa 1 jioni. Mungu na akubariki sana, na uwe na ule moyo wa wepesi wa kufika katika ibada zetu za kila siku hapa kanisani.