MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

14.05.2017: WAZEE WA KANISA NA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAMZAWADIA MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE (MBUNGE) ZAWADI SIKU YA MOTHER'S DAY


Katika siku ya Mother's Day - Jumapili 14.05.2017 wazee wa kanisa  la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kutoa zawadi mbalimbali kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (Mbunge) na kumpongeza kwa malezi bora ambayo amekuwa akifanya kwa waumini wa kanisa hilo kwa miaka mingi. Waumini wa kanisa hilo la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wamekuwa wakipata chakula cha Rohoni na Neno la Mungu ambalo limefanyika baraka kwa walio wengi katika familia zao na maisha yao kwa ujumla. Waumini wengi wa kanisa hilo wamekuwa wakihudumiwa  kimwili na kiroho na hii imesababisha maisha yao kuinuka kutoka chini kwenda juu. Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare amekuwa akisaidia wagonjwa mahospitalini, wafungwa gerezani, wananfunzi, wananchi kupitia utumishi wake serikalini kama mbunge kwa awamu mbili.  Kutokana na mchango wake kwa jamii, waumini wakaona ni vyema kumpongeza kwa zawadi mbalimbali kama alama ya UPENDO kwake. 

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (Mbunge) amekuwa akisaidia jamii kimwili na kiroho bila ya kuangalia dini ya mtu, kabila la mtu, rangi ya mtu, umaarufu wa mtu, taifa la mtu, bali yeye anachojua ni kumsaidia kila mtu kutokana na hitaji lake. Pia amekuwa akijitoa kuwasaidia watu waliofiwa na ndugu zao, wajane kwa kuwatembelea na kuwatia moyo ili wasonge mbele.

Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ni moja ya makanisa ambayo yamefanyika baraka sana katika kuwatia moyo watu waliokata tamaa, kuwahubiria habari njema ya Kristo, kuwainua Kiroho, kuimarisha imani za watu, kufundisha Neno la Mungu, kuwaombea wenye uhitaji, kutatua migogoro ya watu kwa kuwapa ushauri bora na pia kuwaongoza watu katika njia sahihi ya kufika mbinguni kwa Baba.

Inawewzekana na wewe ungetamani kufika hapa kanisani, ibada zetu siku ya Jumapili zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki zinaanza saa 9 mchana hadi saa 1 jioni. Tunakukaribisha sana katika ibada ya Jumapili hii. Mungu atakwenda kuongea na wewe na kutatua shida yako kupitia watumishi wake. Hakuna jambo asiloliweza Mungu kwa mwanandamu, ni wewe kujiweka tayari kupokea mema kutoka kwa Mungu. Unatakiwa kuwa na imani, kujitakasa na kuungama dhambi zako   ili uweze kupokea kile ambacho Mungu anataka upokee kutoka kwake. Ubarikiwe sana


Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (Mbunge)