30.04.2017: WAGENI KUTOKA AFRIKA KUSINI WALIVYO WEZA KUPATA NAFASI YA KUWASALIMIA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIK. "B"

Mh. Mary Mwanjelwa katika ibada ya Tamasha la Maombi iliyofanyika siku ya Jumapili 30.04.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kuwasalimia waumini wenzake wote wa kanisa hilo pamoja na wageni waliofika kwaajili ya maombezi. Pia aliweza kuwakilisha salamu kwa kanisa kutoka Wabunge na watumishi wa serikali waliopo Bungeni Dodoma. Mh. Mary Mwanjelwa aliwashukuru wababa na wamama wa kanisa la Mlima wa Moto waliokuja kumsindikiza Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare katika kuapishwa kuwa Mbunge. Alisema kuwepo kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare Mungu ameweka kwa makusudi kwahiyo tunahitaji sana kumuombea kwasababu kwa kitendo cha kuteuliwa tayari ametangaza vita na shetani na maadui zake, kwahuyi anahitaji msaada wa Mungu.