RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Haki za Binadamu Yazindua Taarifa Yake ya 2016

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Eusebia Munuo, akisoma hotuba yake.

…Akizindua taarifa ya Haki za Binadamu ya LHRC ya mwaka 2016.

Mtafiti wa LHRC Paul Mikongoti, akizungumza jambo katika hafla hiyo.

Baadhi ya wageni mbalimbali.
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali.

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) leo kimezindua taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini katika mwaka 2016.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa ambapo mgeni rasmi alikuwa jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Eusebia Munuo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Munuo alikipongeza kituo hicho kwa kutoa taarifa hiyo kila mwaka akisema kuwa hicho ni kipimo kizuri kwa uwajibikaji, kulinda na kutetea haki za binandamu nchini.

“Tunapozindua taarifa hii ya haki za binadamu ya 2016 tunajielekeza kutazama mwelekeo wa hali ya haki za binadamu nchini kwetu, tunalifanya hili tukiangalia matukio yanayohusu haki za binadamu nchini kwa kutazama wajibu wa wananchi wa kawaida na dola katika kuhakikisha kuwa hali ya haki za binadamu inaborehswa inchini,” alisema.

Naye mtafiti wa kituo hicho, Paul Mikongoti, alisema ni vizuri kuheshimu haki za makundi maalum ambayo ni ya wanawake na watoto, wazee, watu wenye ulemavu, wakimbizi na makundi mengine.