MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

KIONGOZI WA MAKHIRIKHIRI AOKOKA |V.I.TZ


Kiongozi wa kundi maarufu la Nyimbo za Asili la Makhirikhiri la nchini Botswana, Mosesi Malapela a.k.a Shumba Ratshega, ametangaza kumrudia Mungu baada ya kuokoka na kuanza
kuhubiri neno la wokovu. Habari za uhakika kutoka kwa Msemaji wa Kundi la Makhirikhiri Tanzania, Livingstone Mkoi zilieleza kuwa, kwa sasa kiongozi huyo amezaliwa upya
baada ya kuachana na kila kitu cha kidunia na kuamua kumtumikia Mungu
katika maisha yake. Livingstone alifunguka:


“Ni kweli Shumba amenieleza kuwa niwaambie Watanzania kuwa anawaheshimu na kuwakumbuka kutokana na mapokezi
makubwa waliyompa mwaka 2010 alipofika Tanzania kufanya matamasha yake yaliyoandaliwa na Kituo cha Radio Times FM na kumpa mafanikio makubwa. “Shumba anasema kuwa katika maisha yake mapya ya utumishi wa Mungu amekuwa akiiombea sana Tanzania pamoja na Rais Dk. John Pombe Magufuli. “Kuhusu kuimba anasema ataendelea kuimba tu na kundi lake halitakufa kwa
vile ule ni utamaduni wao wa asili.” Mkoi aliongeza: “Tayari mtumishi huyo ameanza ujenzi wa kanisa lake kubwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo (Gaborone) kwa ajili ya kuhubiri Neno la
Mungu.


VIDEO