RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Waziri Kijana Zaidi wa Somalia Auawa kwa Kupigwa Risasi



MOGADISHU, SOMALIA: Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini Somalia, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu muda mchache baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma.

Abas Abdullahi Sheikh Siraji, hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia, kwani alipata umaarufu 

Amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea nchini mwake mwaka jana alipokwenda kwa ajili ya uchaguzi mkuu.

Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi, huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa viongozi. Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo, tayari wamekamatwa.