RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

04.06.2017: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AKEMEA UTASA WA MAFANIKIO UNAOSABABISHA WATU KUTESEKA, ATOA NJIA ZA KUJIKWAMUA NA UTASA HUO

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 04.06.2017 katika ibada Habari Njema ya Kuvunja Utasa alianaza kwa kusema, Bwana asifiwe sana. Utasa sio kuzaa tu watoto, lakini upo utasa wa kiuchumi, wako watu ambao mwaka nenda rudi wanafanya biashara isiyozaa matunda, wanafanya kazi sana, wanaamka saa 11asubuhi kurudi jioni saa 11 jioni lakini wanafanya kazi isiyo zaa matunda, na wengine wana pesa lakini haizai, watu wanafanya huduma zisizozaa matunda. Tulisema mwezi Juni ni mwezi wa Habari Njema, malaika atakuletea habari njema ya gari lako, ghorofa lako, pesa zako, uliowakopesha watakulipa pesa zako kwa jina la Yesu. Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia, Mungu akawambia zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Yeremia 29:5 Jengeni nyumba mkakae ndani yake, pandeni bustani mkale matunda yake, oeni wake , kazae wana na binti, kawaozeni mabinti zenu wazae wana na binti mkaongezeke huko wala msipungue.Naomba Mungu alibariki neno. Utasa maana yake ni kutoweza kuzaa matunda, kama ni uzazi wa kawaida basi mama hawezi kushika mimba, au baba hawezi kuwa na mbegu za kutungisha mimba huo ni utasa. Tunajua kuwa Sara alikuwa tasa lakini kwa kumuomba Mungu alimpata mtoto Isaka, Rebeka pia alikuwa tasa lakini mume wake alimuomba Mungu akapata mapacha Esau na Yakobo. 

Tutashughulika na wale wameolewa lakini wamekawia kuzaa. Umekwenda hospitalini umepasuliwa au umekunywa dawa au umepewa vidonge lakini bado mtoto hajaweza kuonekana Nataka kukuambia kuwa kwa Mungu yote yanawezekana, pokea mtoto wako kwa jina la Yesu, tumbo la uzazi lifunguke kwa jina la Yesu, pokea mtoto wa muujiza kwa Jina la Yesu, uko tayari kwa Baraka zako?!!! Mungu wetu ni mwema, Mungu wetu yuko kazini. Wokovu maana yake ni lazima mwili wako uokoke na Roho yako. Yapo makanisa mengi wanahubiri sana, wanaombea watu sana, lakini mimi ninachoshukuru katika kanisa letu ni kwamba Mungu anaonekana, tukiomba watu wanapata watoto, pesa, maisha yao yanabadilika, watu wanainuliwa. Yeyote ambaye umeolewa umekawia kuzaa usikate tamaa yupo Mungu anayeleta watoto kwani watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, hata ukimgombeza mke wako unamuonea yeye hana uwezo wa kuleta watoto, watoto anayeletwa na Mungu.

Bwana apewe sifa! Wewe baba ambaye mke wako hazai, unatakiwa umvumilie mke, uwe na hekima, mfanye maombi ili muweze kupata mtoto wenu. Mungu anauwezo wa kutungisha mimba na ana uwezo wa kuzalisha watoto. Hata kama umekawia kupata watoto, watoto watakuja tu maana ni zawadi kutoka kwa Mungu, naona zawadi yako ya mtoto inakuja, mjukuu wako anakuja kwa jina la Yesu. Mimi naona wajukuu wako, watoto wako katika jina la Yesu.. “Pokea furaha katika nyumba yako!!!”. Tumesema utasa sio watoto tu lakini kuna UTASA WA KIUCHUMI, watu wanatafuta pesa, lakini wakizipata hawazishiki, zinaruka, zinayeyuka zinaisha. Utasa kiuchumi ni mbaya. Unaweza kupita buchani ukaona nyama ukatamani lakini huna pesa, unapita tu na kujifariji kwa kusema, “Nyama zenyewe malendalenda tu” kumbe hauna hela ya kununulia. Ibada ya leo ikupatie pesa, ifungue milango ya baraka. Nakutamkia baraka leo, nakupa mashilingi kwa jina la Yesu, biashara yako izae matunda kwa jina la Yesu, baraka za watoto zinakufuata. UnajuaTatizo la dunia hii kwa sasa ni pesa, wataalamu wanasema, “Sasa hivi kumekuwa na shida, kumekuwa na ugonjwa wa uchumi umeingia kila mahali, watu wanalia, wanahangaika, na wale walioajiriwa ni kama hawana kazi, waliokuwa na biashara ni kama hawana biashara, wanaoenda kushinda kwenye maduka wanarudi bila pesa, lakini leo kama mtumishi wa Mungu, nang’oa kila pando la uchawi lililopandwa kwenye biashara zetu, tunang’oa halina mamlaka katika jina la Yesu, kwa maana kila pando lisilopandwa na Mungu litang’olewa, kila pando la utasa katika biashara yako, katika kazi ya mikono yako leo tunailaani. Mimi ni mama yako, mimi ni ndugu yako ningependa kukutoa kwenye matatizo. Natamka uchumi kwa kila mtu uweze kuchanua, ulikua mfanyakazi basi Mungu awape vyeo muongezewe mishahara kwa jina la Yesu. Nenda ukahesabu pesa mpaka ulale juu ya noti. 

Bwana Yesu asifiwe. 
Mwambie mwenzako wewe ni mlinzi, mimi mchungaji ni mlinzi wako, mzee wa kanisa pia ni mlinzi wako, wewe pia kama muumini wa kanisa ni mlinzi wa mwenzako, Mungu alimuuliza Kaini, ”Ndugu yako yuko wapi?” Akasema “Kwani mimi mlinzi wa ndugu yangu?” akamwambia, “Ndio na wewe vilevile ni mlinzi wa ndugu yako”. Na wewe muombea ambaye hajafika ibada au yule mgonjwa. Wew ni mlizni wa mwezakao.