RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.06.2017: MH. DR. GERTRUDE RWAKATARE AKIOMBEA WATU WALIOFIKA IBADANI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Nikuombee...Ee Roho Mtakatifu umguse kijana yule, mtoto yule, ama yule, kaka yule, dada yule na mzee yule. Watembelee Mungu wa mbinguni, watu wako wamekuwa na matarajio kutoka kwako kuwa leo ni mwisho wa matatizo yao. Nakuomba Mungu uwatimizie haja ya mioyo yao. Angalia wanavyoteseka na magojwa, ada za shule, kodi za nyumba, mahusiano, kusengenywa, utasa na mengine kama hayo Baba. Nakuomba Mungu uwavute kilio chao siku ya leo. Baba nimeomba na kushukuru Amen.

Nikupongeze wewe uliyeshiriki nasi katika ibada ya NEEMA YA KUANZA UPYA siku Jumapili 11.06.2017, Mungu azidi kukutendea mema maana ujio wako umemfurahisha Mungu na sisi wanadamu tumebarikiwa sana. Tunakuomba sana uzidi kuhudhuria ibada zetu za Mlima wa Moto Mikocheni "B" kila Jumapili saa 3 asubuhi na katikati ya wiki saa 9 mchana


Nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi na tutamaliza saa 8 mchana. Hii ni siku yako ambayo Mungu anataka kuongea na wewe na kukubariki. Jitahidi sana kuhudhuria. Njoo na ndugu na rafiki siku hiyo

//Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Ibada ya 11.06.2017//
Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare