MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

11.06.2017: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AGUSWA NA IMANI YA MUUMINI WAKE


Huyu mama wakati Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akicheza katika ibada ya Jumapili 11.06.2017 ya NEEMA YA KUANZA UPYA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", alijitokeza na kuomba awekewe mikono ili aombewe na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Bishop naye hakuweza kusita ikabidi aahirishe kucheza na kusimamisha msululu uliokuwa nyuma yake na kuanza kuomba naye.

Jamani hii ni IMANI ya tofauti sana. Mama huyu amekuwa na mazoea ya kutaka kila wakati kuombewa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, na akishaombewa mambo yake yanamyookea. Hii ni faida kubwa sana ya kutambua thamani ya mtumishi wako katika maisha yako. Ukijua alichonacho mtumishi wako na ukayaamini yale anayofundisha na kutii, utakula mema ya nchi. Huyu mama anakula mema ya nchi baada ya kuona mbegu iliyomo ndani ya mtumishi wake kuwa ina nguvu ya kutoa matunda bora katika maisha yake na ndio maana ameng'ang'ania kuwekewa mikono na kuombewa.


Bishop aliguswa sana na kitendo cha mama huyu ambaye ni muumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Na wewe unayo nafasi ya kumshirikisha mtumishi wako katika mambo yako unayoyafanya ili akuombee UFANIKIWE. Jijengee tabia ya kuwashirikisha watumishi wako katika mambo yako, kwani hao wamebeba kitu kwaajili yako kutoka kwa Mungu. Wao ni mabalozi wa Mungu.

/ /SASA NAOMBA U-SHARE, LIKE NA COMMENT kwa UTUKUFU wa BWANA.//

//Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Ibada zetu siku ya Jumapili ni saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ni saa 9 mchana//

//Facebook: Mountainoffire Tanzania au Bishop Gertrude Rwakatare //
//Youtube andika Mlima wa Moto au Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola utaona magari yetu na watu wakisema kanisa kwa Mamam Rwakatare..Ingia humo//