RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.06.2017: SHUHUDA: AMSHUKURU MUNGU KUPATA TSHS. 200,000 NA PIKIPIKI

KAZINI KWAKEMuumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 11.06.2017 aliweza kumshukuru Mungu kwa kupata pikipiki ofisini kwake na kulipwa mshahara wa 200,000, alisema; Napenda kumshukuru Mungu kwanza kwa uongozi wa vijana, mwenyekiti wa vijana, Damas katibu wa vijana Charles pamoja na uongozi mzima wa vijana na Victor Williamu Mungu awabariki sana. Mimi nahusika na CCTV kama “Controler.” Mimi na wafanyakazi wenzangu shida yetu kubwa ililikuwa ni mshahara, lakini Mungu alichokifanya katika siku 40 na maombi na kufunga kimeshangaza. Kuna kipindi kazini tulikuwa tunatuma “email” zetu kwa viongozi wetu na hazijibiwi. Tulifyohamia Kigamboni kikazi Mhindi mmoja aliingiza mwanamke kwenye nyumba ya ofisi, sasa mimi nili- “record” walichokuwa wakifanya nika -“save” kwenye “system” na baadae nilimuonyesha “boss”. Kuanzia hapo akaanza kutuamini. Siku moja tukamueleza ”Boss” wetu kuhusu mishahara kuongezwa, naye alikubali kutuongezea. Na baada ya miezi mitatu ikaja tena nafasi nyingine kazini, tukakaa kikao “Boss” akatuuliza; Mnataka niwape shilingi ngapi? tukamwambia tunataka Tshs. 500,000, boss akasema, Mbona hiyo pesa ni nyingi sana, mnaonaje nikawapaTsh. 200,000 na nikawapa na pikipiki. Baada ya muda tukapata pikipiki na mshahara wa Tsh. 200,00. na jambo linguine ambalo likafuata boss ametuwekea ukingo kwamba tusiguswe na mtu yeyote zaidi yake hili ni jambo ambalo namshukuru Mungu kwa hili ongezeko ambalo Mungu ameniongezea. UBARIKIWE