MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

11.06.2017: WALIOKOKA SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KATIKA IBADA YA NEEMA YA KUANZA UPYA


Mungu azidi kukubariki na kukulinda wewe uliyeamua kuokoka siku ya Jumapili 11.06.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ukaongozwa sala ya toba na Mch. Naoha Lukumay na baadae kuombewa na kubatizwa kwa maji mengi.

Unatakiwa kutambua kuwa Mungu alikuwa na mpango na wewe tangia ukiwa mdogo, na leo ameweza kukuokoa katika shimo la mateso na taabu za shetani.

Maamuzi uliyofanya ni maamuzi ya hekima na utukufu mbele za Mungu. Wapo watu wengi wanatamani kuokoka lakini bado wamefungwa na nguvu za giza, ila wewe Mungu alikupa nuru ya kuona njia sahihi ya kwenda mbinguni.

Kwahiyo jitahidi sana kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kila siku, ishi maisha ya toba, maisha ya kufunga na kuomba, maisha ya upendo, maisha ya kushiriki ibada, maisha ya kusoma Neno la Mungu na kuliishi, maisha ya kusaidia wenye uhitaji wa kimwili na kiroho, maisha ya utoaji katika nyumba ya BWANA, maisha ya kuthamani kanisa lako na watumishi wa Mungu waliokuombea leo na watakaozidi kukulisha chakula cha BWANA. Epukana na makundi mabaya, ikimbie dhambi, acha kutamani maisha yako ya zamani kabla ya wokovu. Pale unapopitia magumu, muite Mungu na kuwashirikisha watumishi wake ili wakusaidie. JIAMINI na JITHAMINI katika maisha yako haya ya wokovu.

Katika maisha haya ya wokovu, nakuomba na wewe ukawe balozi wa kuwaleta watu kwa Yesu ili nao waokoke wawe kama wewe. Mungu amekuita kwa makusudi, na kusudi mojawapo ni wewe kuwa kama MVUVI, kuwavua watu na kuja kwa YESU KRISTO kwa njia mbamlimbali.

Leo hii umempokea BWANA kuwa MWOKOZI wa maisha yako na pia ROHO MTAKATIFU ameingia kwako ili akuongoze katika maisha yako ya wokovu, basi usikubali shetani akaingia kwako na kuaharibu hekalu la Mungu lililondani yako. Siku utakaporuhusu tu shetani kuingia ndani ya maisha yako, nakuambia CHAMOTO utakiona, adhabu kubwa utaiona na utajutia kwanini uliamua KUACHA wokovu. Nisikitishe sana ila huo ndio ukweli.

Basi jitahidi Jumatatu na Jumanne kuhudhuria mafundisho ya kukulia wokovu hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 10 jioni. Mungu akubariki na akulinde mwanangu.

// SASA NAOMBA U-SHARE, LIKE NA COMMENT kwa UTUKUFU wa BWANA.//

//Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Ibada zetu siku ya Jumapili ni saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ni saa 9 mchana//
//Tembelea www.mountainoffiretanzania.blogspot.com//
//Facebook: Mountainoffire Tanzania au Bishop Gertrude Rwakatare //
//Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola utaona magari yetu na watu wakisema kanisa kwa Mamam Rwakatare..Ingia humo//