RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.06.2017: WATU WAZIDI KUMIMINIKA KWA YESU NA KUOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Si kitu RAHISI lakini leo kimekuwa RAHISI kwako wewe uliyeamua kuokoka siku ya Jumapili 11.06.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Jambo ulilofanya limempa Mungu heshima na utukufu. Mungu atakwenda kukuheshimisha kwa wanadamu na maadui zako wataabishwa, maana utapokea baraka na MAFANIKIO ya kimwili na kiroho kutoka kwa Mungu mwenyewe.
Kitendo cha kuongozwa sala ya toba na kuombewa na Mch. Noah Lukumay ni moja ya njia ya wewe kuanza maisha mapya yenye furaha na amani. Leo hii umefanyika mpya kwa maana umeungama dhambi zako na ukakubali kubaitizwa kwa maji mengi. Hakika utaenda kuona mkono wa Mungu katika maisha yako kwa Jina la yesu Kristo.


Sasa nenda ukaulinde WOKOVU wako kwa kutenda mema kwa watu wote, kwa kumtumikia Mungu kwa akili zako na mali zako, kwa kuwasaidi watu wengine kuja kwa Yesu, kwa kushika amri za Mungu na kuzifanyia kazi, kwa kulisaidia kanisa lako kupitia karama zako na vipaji ulivyonavyo, kwa kutenda yalio mema mbele za Mungu na mbele za wanadamu, kwa kuomba na kufunga, kwa utoaji katika nyumba ya BWANA, na mengine kama hayo.


Mungu amekupendelea na amekupenda, kwahiyo tunza bahati hii kwa kumtumikia. Jiulize ni watu wangapi wanakufa katika wakiwa waovu na hawajabatizwa? Je, hatma yao ni nini baada ya kifo? Mwanangu unatakiwa kujua kuna watu wanatamani sana kuchukua HATUA kama yako lakini wanashindwa, kwahiyo kuanzia sasa anza kuwaombea kama walivyokuwa wanakuombea watu wa Mungu kabla haujaokoka.


Jitahidi kuhudhuri madarasa ya kukulia wokovu siku ya Jumatatu na Jumanne hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 10 jioni. Masomo haya yatainua kiwango chako cha imani na utajua jinsi ya kulinda wokovu wako kipindi chote utakachokuwepo hapa duniani.


// SASA NAOMBA U-SHARE, LIKE NA COMMENT kwa UTUKUFU wa BWANA.//
//Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Ibada zetu siku ya Jumapili ni saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ni saa 9 mchana//
//Facebook: Mountainoffire Tanzania au Bishop Gertrude Rwakatare //
//Youtube andika Mlima wa Moto au Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola utaona magari yetu na watu wakisema kanisa kwa Mamam Rwakatare..Ingia humo//