MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

11.06.2017:MARTHA KOMANYA ALIVYOONGOZA KIPINDI CHA SIFA KATIKA IBADA YA "NEEMA YA KUANZA UPYA" MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hakuna mtu asiyependa kusifiwa, kila mtu anatamani kuona anapewa sifa kutokana na matendo mema anayoyafanya. Mungu wetu ametundea mambo mengi mazuri katika maisha yetu. Mungu wetu ametulinda, ametupa kazi, watoto, afya njema, magari, majumba, ajira, elimu nzuri, vyeo, miradi, mifugo, mashamba, maeneo ya biashara, wateja wazuri, amani katika taifa n.k. Mungu amekuepusha na ajali, magonjwa, utasa, kusengenywa, kuonewa, laana, mikosi, balaa, mapepo, majini, roho chafu, kuchanjwa usiku, kufeli masomo yako, kufukuzwa kazi na mengine kama hayo. 

Lakini kuna wengine bado wanapitia changamoto nyingi za maisha wakati wewe unafurahia wema wa Mungu. Wapo wanaolia kwa kukosa, ada, kodi ya nyumba, ajira, kazi, chakula, watoto, pesa, amani katika ndoa zao, wachumba wa kuwaoa, wapo wanakosa amani katika majumba yao na mengine kama hayo. Hata kama Mungu amekubariki bado unahitaji kumsifu na kumwabudu, hata kama unaona bado maisha yako ni ya dhiki na unapitia mapito magumu makubwa, lakini bado unahitaji kumsfu Mungu wetu. Unatakiwa kujiuliza kwanini bado unashi wakati wenzako wameshakufa? Mungu ana mpango na wewe. Nikupongeze mtumishi Martha Komanya na Janeth Urasa kwa kutuongoza katika kipindi cha sifa Mlima wa Moto Mikocheni “B” mkishirikiana na Praise and Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” katika ibada ya “NEEMA YA KUANZA UPYA siku ya Jumapili 11.06.2017. Mungu awabariki: //Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare/