MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

SHUHUDA: NEEMA ENOCK BAADA YA KUTESEKA NA WAGANGA WA KIENYEJI APATE MTOTO AIOMBEWA MHE. BISHOP DR. G. RWAKATARE NA SASA ANA MTOTO

Muumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”, Bi. Loveness siku ya Jumapili 11.06.2017 katika ibada ya “Kuliombea Taifa la Tanzania aliweza kumshukuru Mungu na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuweza kupata mtoto baada ya mahangaiko ya muda mrefu, alisema, “Bwana Yesu asifiwe. Napenda kumshukuru sana Mungu, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na mch. Noah Lukumay, wachungaji, washirika wa Mlima wa Moto Mungu kwa maombi yao, wamenisaidia toka nilivyokanyaga kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni ”B” sijawahi kuumwa tena kwanikipindi cha nyuma kabla sijaanza kuhudhuria ibada za hapa nilikuwa naumwa sana, nikishika mimba inaharibika (inatoka), nilikuwa naenda kwa waganga wakienyeji ili nipate mtoto lakini sikufanikiwa , lakini nilipoombewa na Mtumishi wa Mungu Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, hakika Mungu kupitia yeye akavunja utasa wangu nikapata mimba. Nimeenda kwa waganga mara nyingi mganga wa kienyeji alikuwa anatwambia tupeleke kuku, tukaoge baharini, lakini baada ya kuchoshwa na hali hiyo isiyo na mafanikio nikasema nikasema siendi tena, na huyo kuku sipeleki, ndipo nikaamua kuja kanisani. Ninamshukuru Mungu nikapata mimba na leo nimepata mtoto wa kike anaitwa Loveness..