MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

02.07.2017: HAPPY KWAYA NA JOYBRINGERS KWAYA ZA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" ZILIVYOMTUKUZA MUNGU SIKU YA JUMAPILI

//Umenitia furaha moyoni mwangu - Zab 4:7//
//Katika amani nitajilaza na kupata USINGIZI mara, maana Wewe BWANA, pekee yako ndiwe unijaliaye kukaa salama -Zab. 4:8//

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa yale aliyoyafanya katika uzinduzi wa Semina ya siku 8 ya MID YEAR CROSS OVER 2017 iliyoanza rasmi siku ya Jumapili 02.07.2017 na itahitimshwa Jumapili 09.07.2017. Tuliona mkono wa Mungu kupitia waimbaji wa Happy Kwaya na Joybringers Kwaya. Watu tulifurahi ndani ya mioyo yetu na tuliporudi majumbani mwetu tulijawa na nguvu ya Mungu ndani yetu.
Hawa waimbaji wamefanyika baraka kwa waliobahatika kuwasikia kutokana na uimbaji wao na ujumbe wanaoutoa kwetu. Nyimbo zao zina upako wa aina yake, na kama mtu utachukua ule ujumbe wanaouimba, hakika maisha yako yatabadilika.
Kumbuka ya kuwa semina hii ilizinduliwa rasmi na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwashirikiana na Bishop Dunstan Maboya kutoka Arusha na Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda. na semina hii bado inaendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 1 usku. Ni semina ya kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake tangia januari hadi Juni, kwani ametuepusha na mengi mabaya, na pia ni semina ya kukabidhi ya maisha yetu kwa Mungu kwa miezi 6 ijayo kwani kama wanadamu hatujui lililo mbele yetu. Kwahiyo unakaribishwa sana tena sana.

//Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"//

JOYBRINGERS KWAYA
HAPPY KWAYA

0