MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

02.07.2017: PICHA YA PAMOJA YA WATUMISHI WA MUNGU KATIKA UFUNGUZI WA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER 2017 - MLIMA WA MOTO WA MIKOCHENI "B"

Bwana apewe sifa wana wa Mungu. Leo ikiwa ni Jumapili ya kwanza ya mwezi wa saba (02.07.201) ilikuwa ni siku ya baraka sana katika ibada ya UFUNGUZI wa Semina ya MID YEAR CROSS OVER 2017 iliyofunguliwa rasmi na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa na Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda. BWANA aligusa mioyo ya watu kupitia Neno lake lililotolewa na watumishi wake. Hakika Mungu wetu ni Mungu wa huruma, Mungu wa upendo, Mungu anayefariji, Mungu anayeponya, Mungu wa yatima, Mungu wa masikini, Mungu wa matajiri, Mungu asiye na ubaguzi, Mungu anayependa kila mtu. Leo hii amefanyika baraka katika semina ya Kumshukuru Mungu kumaliza miezi sita tangia mwaka uanze na kumkabidhi Mungu kwa miezi sita iliyo mbele yetu.

Wazee wa kanisa, watumishi wa Mungu mbalimbali, wachungaji waliweza kupiga picha ya pamoja kwaajili ya UTUKUFU wa Mungu.

Wewe ambaye hukubahatika kufika katika semina hii siku ya leo, unayo nafasi kubwa sana ya kupokea BARAKA za Mungu kwani semina hii itahitimishwa Jumapili ijayo ya tar. 09.07.2017. Siku ya katikati ya wiki semina itakuwa inaanza saa 9 jioni hadi saa 1 jioni. Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda watakuwepo kukuhudumia...USIKOSE Kabisa...!!

0