RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

02.07.2017: WATU WALIOBATIZWA KATIKA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER - MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza semina ya MID YEAR CROSS OVER ambayo ilianza siku ya Jumapili 02.07.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", watu wengi sana waliweza kuokoka na kumpokea Yesu Kristo kuwa BWABA na Mwokozi wa maisha yao. Mch. Francis Machichi, Mch. Noah Lukumay waliongoza sala ya toba na kuwaombea. Baada ya kuombewa walipewa fomu za kujiunga na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na baadae walibatizwa kwa maji mengi. Wakati wakibatizwa baadhi yao walitokwa na mapepo na majini. Walimpokea ROHO MTAKATIFU. Siku ya Jumatatu na Jumanne waliendelea na masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Sasa, ni wajibu wetu wa kuwaombea hawa ndugu zetu ili wadumu katika wokovu. Kumbuka na wewe ulivyokuwa unaokoka kuna watu walitenga muda kwaajili ya kukuombea, sasa, leo hii ni zamu yako ya kuwaombea hawa ndugu zetu ili shetani asiwateke tena na wakarudi nyuma kufanya maovu. Kumbuka sisi ni mabalozi wa Mungu kwahiyo ni wajibu wetu kuona watu wanaokoka na wanadumu katika wokovu. Unapo bahatika kuwa nao jaribu kuwatia moyo na kuwafundisha Neno Mungu ili imani yao IKUE na KUONGEZEKA na wawe na ujasiri katika kumtumikia Mungu. Kipindi hiki ni kipindi kibaya sana kwao, kwani ni kipindi ambacho shetani kupitia wanandamu na changamoto mbalimbali za kimaisha atatumia kuwavuruga ili wamtumikie yeye na kumuacha Mungu waliomkimbilia.

Pengine na wewe umeguswa na tendo hili na unahitaji kuokoka, basi usikose kufika katika semina inayoendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 1 jioni . Bishop Dunstan Maboya, Mch. Noah Lukumay, Mch. Daniel kalege kutoka Uganda na jopo la wachungaji wa Mlima wa Moto watakuwepo kukusaidia ili uweze kuokoka na kubatizwa. Siku ya Jumapili 09.07.2017 semina hii itahitimishwa rasmi, na siku hiyo semina itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Kumbuka semina hii ni kwaajili ya kumshukuru Mungu kwa miezi sita iliyopita kwani Mungu wetu ametulinda na mengi na ndio maana bado tupo tunaishi, pia ni kwaajili ya Kuvunja vunja kaza za shetani na mpingo mibaya ambayo maadui zetu wameiweka kwa miezi sita ijayo. Ni semina ya kukabidhi maisha yetu kwa Yesu Kristo kwaajili ya ulinzi kwa miezi sita ijayo.



































































Comments