MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

02.07.2017: WATU WALIOOKOKA SIKU YA JUMAPILI YA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER 2017 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayofanya katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Siku ya Jumapili .02.07.2017 watu wengi sana waliweza kuokoka na kuongozwa sala ya toba na Mch. Francis Machichi. Jopo la wachungaji wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kuwaombea na baadae waongofu wapya walibatizwa kwa maji mengi  
Siku ya Jumatatu na Jumanne wataanza masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B

Wewe ambaye hukubahatika kufika siku ya Jumapili, unaalikwa katika semina ya MID YEAR CROSS OVER 2017 inayoendelea leo Jumatatu hadi Jumapili 09.07.2017 saa 9 alasili had saa 1 usiku. Hii ni semina ya kumshukuru Mungu kwa miezi 6 iliyopita na kumkabisa Mungu maisha yetu kwa miezi 6 iliyobaki kumaliza mwaka, pia kutaka na maombezi kwa watu wenye shida mbalimbali kutoka kwa Bidhop Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege  kutoka Uganda. Kwahiyo wahi mapema ili uweze kupokea baraka za Mungu kupitia watumishi wake

Mch. Francis Machichi akiongoza sala ya toba
0