RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

02.07.2017: WATU WAFUNGULIWA KUPITIA KIPINDI CHA KUSIFU NA KUABUDU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

//Mwimbiyeni BWANA akaaye Sayuni, yatangazeni kati ya watu matendo yake//

Wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" na wageni waliofika katika uzinduzi wa semina ya siku 8 ya MID YEAR CROSS OVER 2017 uliyofanyika Jumapili 02.07.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kumuimbia BWANA kama Zaburi 9:11 inavyosema wakimtukuza kwa yale waliyotendewa kwa miezi sita iliyopita. Martha Komanya na Praise & Worship Team wa kanisa hili waliweza kumtukuza Mungu kwa vinywa vyao kwa kupaza sauti kwaajili ya BWANA. Watu wengi waliguswa na nguvu za Mungu kupitia kipindi hiki cha sifa.

Baada ya sifa waumini na wageni waliofika katika kusali mahali hapa waliweza kuingia katika ibada ya kuabudu ambapo watu waliabudu na kuomba. Katika ibada tuliona watu wakiguswa na nguvu za Mungu na wengine wakipeleka haja zao kwa Mungu kulingana na mahitaji yao.

Wewe ambaye hukubahatika kufika kanisani siku ya Jumapili umepewa nafasi nyingine ya kushiriki na wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" katika kipindi hiki maalum cha semina ya siku 8 kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku kila siku, ila Jumapili semina itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Wahubiri ni Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda na Bishop Dunstan Maboya kutoka Arusha

Hizi ni siku za kuvunja milango ya shetani iliyozuia kutofikia malengo yako, kukosa amani, kukosa kodi ya nyumba, kukosa amani katika ndoa, kukosa safari za nje, kukosa kazi, kukosa ajira, kukosa ada ya shule, kukosa uwezo wa kulipa madeni, kukosa afya njema, kukosa, wateja n.k. Mungu anweza, Mungu ni Mungu wa upendo na huruma, atakusaidia. Usijizuie kufika katika nyumba ya BWANA.

 Martha Komanya





































Comments