MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

16.07.2017: MATUKIO KATIKA PICHA ZA IBADA YA KUPELEKA MASHITAKA KWA MUNGU

Siku ya Jumapili 16.07.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"katika ibada ya "Kupeleka mashitaka yetu kwa Mungu" Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay na jopo la wachungaji waliweza kuwaombea watu wenye shida mbalimbali ili Mungu aingilie kati katika maisha yao. Ilikuwa ni ibada ya tofauti sana ambapo watu waliandika mahitaji yao katika karatasi na kuyawakilisha madhabahuni ili yaweze kuombewa. Kila mtu aliandika hitaji lake kulingana na changamoto anazopitia katika maisha yake

Yawezekana na wewe unapitiwa changamoto mbalimbali, umehangaika kwa waganga, makanisa mbalimbali na madhehebu mbalimbali lakini hukuweza kupata suluhisho la mapito unayopitia, umekuwa mtu wa kulia na pengine kumkufulu Mungu pasipo sabaubu, lakini leo nataka nikupe njia sahihi ya kutatua tatizo lako nayo ni kumpokea Yesu kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako. Tamani kila wakati kumshirikisha Mungu katika kila jambo unalolifanya au katika changamoto unayopitia, Pia waamini watumishi wa Mungu kwa kila jambo wanalokuagiza kwa maana wao ni mabalozi wa Mungu hapa duniani. Mungu anaongea kupitia vinywa vyao na akishaongea miujiza inatokea kwako. Tumeona Mungu akimtumia mtumishi wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na watu wamekuwa wakipokea miujiza yao, na hii ni kutokana na watu kutii maagizo wanayoambiwa na mtumishi wake.

Nikualike katika ibada ya Jumapili katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ibada zetu zina anza saa 3 asubuhi hadi saa 8 Mchana na usafiri ni bure kutoka kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.0