MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

16.07.2017: MCH. NICCU KUTOKA MAREKANI AFUNGA SAFARI KUJA TANZANIA KUJA KULIOMBEA TAIFA NA RAIS WA NCHI

Mch. Niccu kutoka Marekani ambaye ni mzaliwa wa Mbeya siku ya Jumapili 16.07.2017 katika ibada ya KUPELEKA MASHITAKA YETU KWA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", alimshukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kumpa nafasi ya kuweza kulisalimia kanisa. Pia alimshukuru Mungu kwa kumlinda mpaka umri huu alionao. Lengo la ujio wake Tanzania akiwa ameongozana na baadhi ya watumishi wa Mungu ni kuliombea Taifa Am la Tanzania amani, upendo na mshikamano. Alisema Tanzania ni ya thamni sana duniani na imebahatika kupata kiongozi bora Rais Dkt. John Magufuli ambaye kwa uongozi wake amekuwa kila wakati akiomba sana watu waweze kumuombewa kwasababua anatambua bila Mungu hawezi lolote.  Mch. Niccu aliweza kusukumwa na Roho Mtakatifu kuja Tanzania kwaajili ya kuliombea Taifa hili na pia kutimiza kile kilio cha Rais cha kutaka kuombewa ili aweze kuliongoza Taifa kwa amani na upendo.

Sasa wewe ambaye ulikosa kusikia au kumuona Mch. Niccu, naomba sana uendelee kufuatilia post zetu wakati tunaanda masomo yake. Na pia tunakukaribisha sana kat0ika ibada ya Jumapili hii saa 3 alasiri hadi saa 8 Mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Ubarikiwe na BWANA
Mch. Niccu kutoka Marekani


 Mh. Marry Mwanjelwa (Mbunge) wa nne kutoka kushoto
Mch. Niccu (kulia) akiwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare)0