MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

16.07.2017: MZEE WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" AMSHUKURU MUNGU KUMUOKOA NA AJALI MBAYA

Mzee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 16.07.2017 alimshukuru Mungu kwa kumuokoa na ajali mbaya aliyopata. Pia aliwashukuru wachungaji na waumini waliomuombea na wanaomuombea kipindi hiki anachougulia mkono wake na mwili wake kwa ujumla.
16.07.2017: MLIMA WA MOTO MIKOCHENI :"B": 
Yawezekana unapitia jaribu hili, ni maombi yangu siku ya leo Mungu wa mbinguni akuponye, akuondolee na maumivu haya, akuondolee na mawazo juu ya ugonjwa wako, Mungu akupe amani na furaha, Mungu akutie nguvu upya. Tuna kemea Roho za uharibu, Roho za ajali, tuvunja kazi za shetani katika familia yako, ndoa yako, elimu yako, biashara yako, taaluma yako n.k. Tunasema, shetani hana mamlaka juu ya mwili wako. Pokea uponyaji kwa jina la Yesu Kristo.

Ninakuomba Jumapili hii saa 3 asubuhi tukutane katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana ili tumlilie Mungu wetu kwa mapito tunayopitia sehemu mbalimbali za maisha yetu. Ni siku ya kuvunja na kuharibu kazi za shetani. Usikose kuja na ndugu au rafiki yako ndani ya hekalu la Mungu. Ni siku yako ya kufunguliwa katika vifungo vya shetani, utakuwa huru na utafurahia wokovu wako, utalindwa kwa damu ya Yesu...

Usafirini bure kuanzia kituo cha Mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye maataa barabara ya Coca Cola, utaona magari yetu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B"
0