RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.06.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIA NA BALAA LA NJAA KWA WATANZANIA WENGI

Siku ya Jumapili 25.06.2017 katika ibada ya KUONDOA NJAA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambapo watu waliweza kuja na mikatate kwaajili ya kuiombea, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema, “BWANA Yesu asifiwe, katika Biblia Yesu anasema, ”Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo mizito, mimi nitawapumnzisha.” Njoo kwa Yesu wewe unayelemewa na magonjwa, madeni, kudharauliwa na kuchekwa Yesu atakupumnzisha. Yesu yuko mahali hapa, kilio chako si cha peke yako, amekuchora kwenye vitanga vya mikono  yake, anakuangalia unavyolia,  unavyodharauliwa, unavyochukiwa bila sababu, unavyoonewa Yesu yupo kukusaidia. Leo ni ibada ya kukomesha njaa katika nyumba zetu. Sijasema umelala njaa au huna pesa, lakini unaweza ukawa unapitia changamoto mbalimbali na hiyo ikawa ndio njaa yako. Kilio cha Tanzania wengi ni njaa,  wanakula mlo mmoja, wengine hata wakitoka kwenye ibada leo hawajui watakula nini? Ukweli ni kwamba pesa zimetoweka, pesa zimekuwa ni bidhaa adimu vitu tulivyokuwa tunavifanya zamani sasa hivi hatuwezi kuvifanya, mtu mwenye Tshs. 100,000 anaweza akakamatwa hata na jambazi, watu wanauwawa kwa Tsh.1,000,000, watu wanapigwa risasa kwa Tsh.500,000 tu, wanafikilia unapesa nyingi, hali ni tete, lazima kama kanisa tuombee ili wote tuwe katika “level” moja. Katika sala ya BWANA, anasema, “Utupe leo mkate wa kila siku.” Yesu alitufundisha namna ya kuomba mbele ya Baba yetu, kwahiyo nimaombi yangu  mlo mmoja ukome kwa jina la Yesu, Mungu akafungue ukurasa mpya, miezi saba inayofuata iwe miezi ya mikate, iwe miezi ya Baraka, iwe miezi ya kula chakula tele na kusaza katika jina la Yesu. Ninachokuomba uzidi kumtumikia Mungu kwa kutenda mema, kuwasaidia wenye uhitaji kwa chochote unachokipata na pia kutenda mema na Mungu atafungua milango ya mafanikio na kuondoa balaa la njaa katika nyumba yako. 

Jamani watu wanateseka kutokana na hali ngumu ya kimaisha, watu hawaaminiani na kama huna pesa unadharauliwa na pengine  kutukanwa. Watu hawakuamini unapotaka kuwakopa, utasikia wakisema, “Nikukopeshe hela utalipa nini hata kazi huna?” Biblia inasema, “Wenye navyo wataongezewa, waliokuwa hawana hata kile walichonacho watanyang’anywa.” Mimi nataka kuwe na mabadiliko, leo tunapindua umaskini  unakwenda kukoma katika jina la Yesu. Anza kumuomba Mungu na  kukung’uta roho ya umaskini katika jina la Yesu, sema,  “Naikataa, roho ya uhitaji, naikataa katika jina la Yesu Kristo. Nimekuja leo kukuombea ili Yesu aweze  kukuhamisha kutoka kwenye umaskini na kukuingiza kwenye utajiri, kutoka kwenye magonjwa uingie kwa watu wenye afya,  kutoka katika hali ya kukataliwa na kudharauliwa uingie kwenye hali ya kuheshimiwa. Unajuahata ukiwa huna elimu lakini una pesa watu watakuita tu mheshimiwa na yule ambaye amesoma na hana pesa automatically watu watamthamini mwenye pesa. Lakini leo ninakutabiria  kwa miezi sita ijayo kumaliza mwaka 2017 itakuwa ni miezi ya mikate (kuondolewa njaa), Mungu anakwenda kutenda katika jina la Yesu. Katika mafanikio si kwamba uwe na vingi ili ufanikiwe  bali hata kile kidogo unachopata  usikidharau, ule mwanzo mdogo ndio utakaokupa vingi. Unatakiwa kuwa na imani na kazi unayoifanya ambaya unafikili itakuletea mafanikio hapo baadaye, uwe mvumilivu katika changamoto unazopata kazini kwako, na ujitahidi kuzitatua kwa wakati sahihi, usikate tamaa, maombi yawe ndio silaha na mafanikio yako, sikiliza sauti ya Mungu na kuitii  kama Musa alivyosikia sauti ya Mungu akachukua fimbo akapiga bahari na bahari ikagawanyika, nao wakapita,   ukisoma katika kitabu cha Kutoka 4:1-5 utaona jinsi Mungu alivyomfanikisha Musa  katika kipindi kigumu alichokuwa anapitia. 





































Comments