MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

ADHA YA KUFUNGWA VITUO VYA MAFUTA YAWAKUMBA WATEJA


Kituo cha mafuta cha TSN kilichopo Bamaga.BAADHI ya watumiaji wa vyombo vya moto kama vile pikipiki na magari wamezungumzia adha ambayo wamekutana nayo leo baada ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuvifungia vituo vya kuuza mafuta kutokana na baadhi ya vituo hivyo kutotoa risiti za mashine za elektroniki (EFD) kwa wanunuzi wa mafuta.


Mtangazaji wa Global TV Online, Isri Mohammed akifanya mahojiano na mmoja wa waendesha bajaji waliofika kujaza mafuta kwenye chombo chake. 


Vituo mbalimbali vya mafuta jijini Dar es Salaam na miji mingine nchini, vimefungwa kutokana na kutoweka mashine hizo kwenye mita za mafuta mnamo siku tatu zilizopita na zoezi hilo linaendelela nchi nzima.


Mahoijiano yakiendelea.


Mmoja wa waendeshaji wa bodaboda kituo cha Bamaga jijini Dar es Salaam alizungumza na mtandao huu akijitambulisha kwa jina la Kengele Mabula alisema amepata usumbufu mkubwa wa kununua mafuta kwani karibu vituo vyote vilivyo karibu yake vimefungwa na hivyo kulazimika kwenda umbali mrefu, hivyo akashauri kama tatizo ni wamiliki wa vituo hivyo kutofunga mashine hizo basi wajitahidi wakae pamoja na serikali na wazifunge kwenye vituo vyao ili kuondoa usumbufu kwa wateja wao.


Kituo cha GBP kilichopo Sinza Mapambano baada ya kufungwa.


Naye Masoud Juma aliyekuwa katika kituo cha mafuta cha maeneo ya Afrika Sana alisema wamiliki wa vituo hivyo hawapaswi kukinzana na serikali inavyotaka kwamba kila mwananchi akinunua kitu apewe risiti ili serikali ipate kodi na hivyo wajitahidi wafunge mashine hizo kuondoa usumbufu.NA DENIS MTIMA/GPL

0