RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

02.07.2017: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWAOMBA WAUMINI WAACHE MANENO MACHAFU YANAYOSABABISHA WATU KUTOHUDHURIA IBADA

Siku ya Jumapili 02.07.2017 Mh. Bisgop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda waliweza kuzindua rasmi semina ya siku 8 ya MID YEAR CROSS OVER 2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Lengo kubwa la semina hii, kwanza ni kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake kwa miezi 6 iliyopita na kumkabidhi maisha yetu kwa miezi 6 iliyo mbele yetu kuumaliza mwaka. Semina hii yenye nguvu za Mungu itaambatana na maombezi ya kufunguliwa kati vifungo vya shetani juu ya maisha yetu. Wapo watu waliofungwa katika ndoa, biashara, afya, kazi, mahusiano, familia, uchumba, kibali, promosheni, masomo, na wengine wamekubwa na roho chafu, majini, mapepo, madeni, kukataliwa, kusengenywa, kutowaheshimu wazazi wao, kutosoma Neno la Mungu, kutoshika amri kumi za Mungu na mengine kama hayo. Kwa kupitia semina hii watu wataenda kufunguliwa katika mapito wanayopitia changamoto mbalimbali. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda wataenda kutoa Neno la Mungu litakalobadilisha historia ya maisha yako kama utaliamini Neno na kulifanyia kazi. 

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare Jumapili hii, aliweza kuhimiza watu kuacha tabia ya kuwasema watu, kuwasengenya, kuleta maneno ya uzushi, kuwashushia heshima watu kwa kuwatamkia maneno yasiyo ya kweli, kuwakatisha tamaa watu kuja kanisani kutokana na maneno machafu yanayoongelewa na watu wachache ndani ya kanisa. Bishop aliweza kuwaonya waache mara moja na kama watashindwa kuacha tabia hiyo, ni afadhari wasije kanisani au waungame dhambi zao mara moja. Akiongea kwa masikitiko alisema makanisa mengi sasa hivi yanakosa watu kutokana na maneno machafu yanayotolewa na waumini ndani ya kanisa, watu wanaona ni afadhari wakabaki nyumbani kuliko kuja kanisani. Aliomba tabia hii iachwe mara moja kwa sababu inasababisha watu kuikosa mbingu.

Sasa, wewe ambaye ulikosa semina hii siku ya Jumapili, unayo nafasi nyingine ya kuhudhuria semina hii katikati ya wiki kuanzia Jumatatu hii mpaka tarehe 09.07.2017 hapa Mlima wa Moto Mikocheni “B” saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku, Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda watakuwepo kukuombea ili miezi sita ijayo BWANA akafungue milango yako ya Baraka na kufunga milango ya mikosi na balaa katika maisha yako.


Bishop Dr.Gertrude  Rwakatare

















 

 









 


























Comments