RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BWANA URIO ASIYE NA MIGUU NA MIKONO LAKINI NI MCHORA MZURI WA RAMANI ZA NYUMBA


Bwana Urio hana mikono wala miguu ila amebahatika sana kuwa na vipaji lukuki. Moja ya kazi anazofanya ni kuchora ramani za nyumba.

Bwana Urio alioa mke wa kwanza ambaye alibahatika kupata watoto nae bahati mbaya watoto na mama walifariki ila mwaka jana ameoa tena mpaka sasa bado yuko na mke wake na ana wivu sana na mke wake.

Bwana Urio anaweza kuimba, anaweza kuchekesha,anaweza kuigiza etc hivi vyote ni vipaji amezaliwa navyo.

Kati ya vitu ambavyo hawezi ni kuomba omba.
Kilichonishangaza zaidi yeye kama mwanaume wa nyumba ana fight kwa sababu ya familia yake ana fight kwa sababu ya mama yake aliye Arusha ana fight kwa ajili ya ndugu zake wengine. Kubwa kuliko amejenga nyumba yake ambayo anaishi na mke wake kifupi tu yeye ni baba mwenyenyumba.

Kutokuwa na mikono haimzuii kutokuwa na simu wala kutuma sms wala kupiga simu kuna uwezo Mungu ameweka kwake kupitia kamkono kadogo ka upande wa kulia. Amesema akikukaba hapo mpaka uite breakdown ndo itakutoa.

Kati ya vitu nina amini tukifika Mbinguni vitakuwepo ni Fimbo za kwenye makalio. Kuna wengi sana tutachapwa malaika fimbo za kutosha kwa sababu tutaanza kusema "Unajua Mungu mimi sikufikia ndoto zangu sababu baba alikufa, sikufanya sababu nilikuwa mfupi, sikufanya hivi kwa sababu kadha wa kadha" ukimaliza kuhadithia Mungu atakuletea akina Urio kama 9 hv ambao hawakuwa na mikono wala miguu ambao wali fight wali fight wakatimiza ndoto zao.

Siku utakayofukuzwa kazi utashangaa kuwa unaweza kuishi bila hiyo kazi, siku utakayoanza kutumia kipaji chako utashangaa kuwa ubaweza ishi bila Digrii yako, siku Utakayoanza tumia Ubunifu Kutumia Taaluma yako utagundua kuwa unaweza kuishi bila kutegemea kupandishwa cheo, mengi unayodhani huyawezi ni kwa sababu tu una njia mbadala.

Usiseme haiwezekani sema tu Hujui.

Comments