MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

Esther Bernard Malikia: MUNGU ANATENGENEZA FUTURE YAKO MSAMEHE ANAYESHIKILIA MAKOSA YAKO YA NYUMA!

Shalom
Nimesikia msukumo sana kuongea na mtu ambaye anahukumiwa kwa makosa yake ya zamani. 
Nataka nikukumbushe pamoja kwamba neno la Mungu linasema utavuna ulichopanda na kwamba mshahara wa dhambi ni mauti ipo sababu ya wewe kuishi kiroho na Kimwili ndio Mana Mungu alikupa neema ya kutambua makosa yako na ukatubu ... 
Ninaelewa kuwa Jamii iliyokuzunguka haiamini kuwa uliyoyafanya nyuma yalikua sign ya kuonyesha kuwa wewe sio MKAMILIFU na ulihitaji msaada wa kutoka hapo kwenye hizo tabia kwa sababu zimekuchosha, hivyo basi watu hawa ni ngumu kwao kukuunganisha na Mungu badala yake wameshikilia makosa yako na scandals zako zote na kukufanya ujutie na uumie isivyoelezeka unashindwa kusonga mbele ukitafakari jinsi ulivyokuwa mpumbavu kuyatenda au kuyarudia hayo makosa yako. Nakueleza ukweli IKIWA UMEAMINIWA NA MUNGU HIYO IMETOSHA! Huwezi kumlazimisha kila mtu akuone jinsi ujionavyo ni wachache watakaojua Badiliko Lako na kusimama na wewe ili ufike mbinguni na hawa ndio wanafaa kuwa rafiki zako katika Kristo.

Watu wengi tunajisahau kuwa hakuna MKAMILIFU, na furaha ya Mungu huja pale kwa mtu anapotambua makosa yake akageuka na kutubu Mungu hufuta na kusahau na kuanza nawe upya.... Napenda nikutie moyo muangalie anayeandaa future yako ijayo maisha yako ya mbele, mwanadamu ANAYESHIKILIA kosa Lako na kusahau yake Mungu atashugulika naye kwa wakati wake, mshukuru Mungu amekutoa huko songa mbele!

Share 
Esther Bernard Malikia0