MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

Esther Bernard Malikia: USIMSAIDIE MUNGU KAZI ALICHOKIPANGA KITATIMIA TU!

Namshukuru Mungu kwa sababu katika baraka anazotupa alishazipanga kabla hajatuumba soma Jeremiah 1:5 na Jeremiah 29:11-13 Mungu anajua anachotuwazia na anajua tutafika hapo alitujua kabla ya yoyote tuliyemkuta duniani kutufahamu huyo ndiye Mungu tunayemuamini.

Inawezekana Mungu ameshazungumza nawe kwa habari ya maisha yako naamanisha kwamba umemuomba kitu fulani na umeanza Kuona mwanga wa jambo Hilo USIHARAKISHE ukatumia kila njia ukafika hapo nataka nikukumbushe cha Mungu hakina haraka, hila, magomvi wala visasi jambo la Mungu hutokea automatically hata kama kuwe na ugumu upi lakini ndani hutojisikia kamwe kukata tamaa na utazidi kumwachia Mungu kazi yake amalize mwenyewe usipite njia za panya wala usivunje utaratibu sababu tu umeshajua baraka fulani ni yako wala haina haja ya kugombana na watu na kuwekeana chuki acha Mungu akupitishe BARABARA HALALI NA SALAMA utafika kwa KISHINDO na kumpa yeye sifa....................

Inawezekana Kuna watu wameshaiona pia baraka yako na hawataki uifikie wameshajua utakapoelekea kimaisha ni penye neema na wanataka kumsaidi Mungu majukumu ya kukupinga kukuwekea vikwazo, uzushi na vikao ili usifike hapo, nakutia moyo USIPOTEZE MUDA KWA WASIOTAMBUA MUDA WA MUNGU juu ya baraka zako relax acha Mungu awe dereva akufikishe pale penye BARAKA ZAKO!

Esther Bernard Malikia
0