MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

KATIKA MAGUMU NEEMA YA MUNGU ITAKUVUSHA HAPO ULIPO ENDELEA KUJITIA NGUVU!


Kuna wakati mwingine maisha unayaona kama hayana maana kwako kabisa, na nataka nikukumbushe kuwa si kila unayesikia ameamua kukatisha maisha yake kwamba hakuwa anamjua Mungu Bali alikosa tumaini na aliishiwa NGUVU za kutaka Kuona hatima yake. Sio tu hivyo watu wengine wanaamua kujidhuru kama kujikatia tamaa kwa sababu hawana NGUVU ya Kuona thamani yao tena! Unaweza ukashangaa kwanini mtu anatelekeza familia yake alikosa NGUVU ya kuhimili majukumu ya familia yake.

Wakati mwingine unaweza kukoswa koswa na kugongwa gari kwa maana unawaza magumu unayopitia huna pesa, huna amani na furaha, biashara zako zinadorora, kila unayemfata kumweleza shida zako naye anakupiga tarehe au ana majukumu, inafika hatua unalia ndani hakuna anayejua wakati mwingine unaweza kupitisha siku Tatu hujala kitu au umeshindia maji au uji, madeni yamekujaa, watoto wanakutazama kwa habari ya ada na chakula hata pesa za matumizi yao unahisi huna NGUVU ya kuendelea machozi yanakujaa na kujuta kwanini ulikuja duniani! Unawaza kufanya maamuzi magumu ya uhalifu biashara haramu Bila kuangalia matokeo mabaya ya waliojaribu kufanya hayo ni kwa sababu huna NGUVU ya kutenda mema tena kwani ulishatendewa ukatili wa kutosha hauoni haja ya kuwa mwema tena kwa mtu yoyote.

Napenda nikwambie kwamba tunapopitia magumu si kwamba MUNGU hatuoni ila anataka kutuona kama tunaweza KUSTAHIMILI kumtegemea yeye katika magumu na akiona tumefika hiyo level ndio anatuma NEEMA Yake kututoa hapo na kutufuta machozi, Na hiyo NGUVU ya kushinda inatoka kwake na msingi wake ni IMANI Mungu akusaidie usimuache hata iweje UTATOKA KATIKA
HAYO MAGUMU UNAYOPITIA!

Esther Bernard Malikia
Barikiwa


0