MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

Luciana Kambo: WAJIBU WA MWANANUME KATIKA NYUMBA YAKE1Timotheo 5:8

Mwanaume wajibu wako mkubwa ni kuhakikisha kuwa nyumbani kwako kuko vizuri, yani mke wako unampenda na kumtunza vema na watoto pia, wanakula , wanavaa na wanasoma vizuri na wanapo pa kuishi, huko ndio kutwa mume yani umekamilika kila idara kwa habari ya familia yako na kamwe hutapungukiwa maana ni agizo moja wapo la Mungu kwa mwanaume ni umpende mke wako na kumtunza sisi kazi yetu ni kuwaheshimu nyinyi na kuwatii.

Sasa akina baba wa sasa hivi wengi wanajisahau sana na kujifanya maandiko hamyajui au mmeyasahau na badala yake mnataka mtelemko yaani mteleze kama ganda la ndizi vile, 
Yaani Kisa mwanamke anafanya kazi au ana biashara inayomuingizia kipato tena wakati mwingine kikubwa kuliko mume basi ndio unarelax kabisa mwanaume unakula bata unamwachia mwanamke majukumu, alishe familia, watoto awavalishe na yeye mwenyewe ajihudumie, tena wengine utawasikia kabisa wakijisifia kwa wenzao kuwa aaaaaaah Mimi mke wangu jembe bwana yaani anakimbiza hatari tena hata aibu haoni, mshahara wako wewe hauoni kabisa kazi yako kuzungusha round huko baa maana una uhakika wa kukuta chakula, na mambo mengine unaona yanaenda tu.

Na wengine bila aibu kabisa wanawalazimisha wake zao wawape hela zao na mshahara wao wote wakae nao na kuanza kuwapangia matumizi,tena wengine pamoja na kuchukua hela zao bado wanawanyanyasa na wanaenda kutumia na wanawake wengine hela za mama wa watu kwa sababu ya utii anashindwa kukataa na mwingine ndio anampenda kafa kaoza anakufa kijeshi jeshi. Hahaaaaaaaaa wewe baba umenipenda Mimi na kunioa au umependa hela yangu au mshahara wangu? Maana iweje uninyanyase hivyo na mshahara au pesa zangu mwenyewe.

Mwanamke sio jukumu lake kuihudumia familia yako wewe ambaye unatakiwa kufanya hilo, yeye kama ana kazi au ndio kipato ana uwezo wa kukusaidia Mme wake kuongezea kipato chenu kwa ajili ya maendeleo yenu wenyewe na ni kwa utaratibu na kwa upendo na siyo kumlazimisha na kumnyanyasa na hela zake Kisa anakupenda sana.huwezi kuona mke wako anapendeza Leo kasuka nywele hizi kesho zile kavaa hii kesho ile hata hujui kanunuaje, watoto hivyo hivyo na wewe upo unaona na hujahusika na chochote halafu una amani kabisa. jamani muwage na aibu kidogo haipendezi. Mwanamke unatakiwa kupendwa, kudekezwa na wakati mwingine hata kama ana hela zake bado anahitaji kupewa hela anjisikia vizuri hata kama ni kidogo, ule upendo wako anauona

Asubuhi ikifika unampa hela ya nauli na kula wewe mwenyewe Kisa mshahara wake kakupa kwani yeye amekwambia hawezi kujipangilia mambo yake, aaaaaaaaaaaaaaaaaaaah acheni kutugandamiza wanawake tunaweza bwana, hiyo mifumo ya unyanyasaji ilishapitwa na wakati bwana, huko nje unajifanya una roho nzuri kweli kidogo tu ukiombwa hela umetoa kutaka kuonekana wakati nyumbani kwako hufanyi hivyo.

Mwanaume mpende mke wako, Mwamini kuwa anaweza chochote na simamia majukumu yako kama mume sasa ukiwa unamwachia yeye wewe utakuwa nani maana yeye tayari ndio anafanya nafasi yako ya kuwa kiongozi wa familia, hata kama ni kidogo hicho hicho mkabidhi mke wako. Atakipangilia na kitatosha tu badala ya kujisifia ujinga huko kijiweni au kwa rafiki zako, anafanya wajibu wako kwa sababu wewe umeshindwa kusimama kwenye nafasi yako kama baba, sasa kuna mwanamke yupo tayari kuona watoto wake wanashinda njaa? Au wanakosa nguo za kuvaa Kisa wewe baba haujitambui na kusimama, hayupo hata mmoja, zaidi zaidi itakushushia heshima kwa mke wako na watoto kwa kutokuwajibika kwako ndio maana wababa wengi wa sasa hawaheshimiki na wake zao moja ya sababu ni hii atakuhehim vipi baba wakati wewe mwenyewe hutimizi wajibu wako.

Wababa mbadilike jamani Mimi nawapenda ndio maana ninawakumbusha haya, heshima ya wewe kuwa mume ni kuwajibika kwa habari ya familia yako na sio kuonekana tu umevaa suruali na shati umependeza basi.ooooooooooooh shauri yenu ifike mahali mke wako amshukuru Mungu kwa ajili yako na sio kusikitika. Asiewatunza wa nyumbani kwake .......................malizia mwenyewe
0