RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

18.06.2017 : MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ATOA YA MOYONI JUU YA RAIS DR. JOHN MAGUFULI


Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 18.06.2017 katika ibada ya kumuombea Rais wa Tanzania, Bunge na Jeshi la Ulinzi alikuwa na haya ya kusema. Bwana Yesu apewe sifa!! Leo tumeiteuwa siku ya kumuombea Rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli, tunamuombea kwa sababu ya ujasiri na mzalendo namba moja. Yale ambayo ameyafanya kwa kipindi kifupi masikio ya majirai na wale adui zetu yanawasha. Kwa kipindi kifupi amegundua mambo mengi ambayo yameleta mabadiliko makubwa katika Taifa letu kwa kuanza tu, amegundua wafanyakazi hewa, ufisadi wa ma-container yanayoenda bila ushuru, vyeti feki, akaleta madenge makubwa, akajenga barabara, dhahabu inayoibiwa kuanzia mwaka 1998 mpaka leo, angalia mambo mazuri yanayotendeka. Rais wetu analia nao wanaolia, anafurahi nao wanaofurahi, anatoa haki kwa walioonewa. Nchi zote jirani wanasaga meno wanasema, “Jamani hongereni Watanzania kwa kuwa na huyu Rais”, rafiki zangu wengi wengine kutoka serikali ya Kenya, Uganda wananipigia simu wanasema, “Mama Rwakatare hongereni jamani kwa kumpata Rais mchapakazi, muombeeni Rais wenu na sisi tungependa lakini hatuko Tanzania.” Jamani Rais wetu ni zawadi kutoka kwa BWANA, ni tunu itakayodumu, anahitaji maombi ya ulinzi. Kazi aliyofanya ni kama kushika ndevu za Simba yaani ni vita, lakini mbele kwa mbele, amejitoa muhanga akasema. poletea pote lakini Tanzania kwanza, tunamshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi nzuri, kwa ajili ya kupendelewa, na mimi naiona Tanzania mpya chini ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na mimi naona sasa ndoto za Mwalimu. Julius Nyerere zimetimia ya kwamba lazima tulinde urithi wa kizazi kijacho hata kama hutaki kutoa pongezi, lakini ukweli wewe mwenyewe umejionea kwa macho ako ndege mkubwa mzungu imekuja Tanzania nay eye mwenyewe akasema tukae mezani tukae na nchi yetu,wapendwa watanzania inatupasa kutoa pongezi za dhati mimi nilikuwa nafikiria maandamano yangekuwa yanatokea kona hadi kona maandamano ya kumuunga rais wetu kwa kazi nzuri ambayo amefanya tusingoje mpaka mtu ameondoka ndo tuseme alikuwa mwema, kama unamaua mpelekee sasa akanuse yu hai, ubishi ukashindwe katika Taifa letu kwa jina la Yesu lakini tumpe heshima anayestahili heshima kwa jina la Yesu, tunamshukuru Mungu kwa ajili ya Rais wetu.





Bishop Dr. Gertrude Rwakatare



 Mch. Noah Lukumay akiwa amenyoosha bendera ya Taifa
 Kulia ni Mhe. Mary Mwanjelwa (Mbunge)


Comments