RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MHUBIRI NICK VUJICIC ATOA ALBAMU YAKE YA KWANZA YA MUZIKI ILI KUENEZA MATUMAINI.





Mhubiri wa Australia, Nick Vujicic alizaliwa bila mikono na miguu, lakini hiyo haikumzuia kuongoza maisha yake kamili. Mhubiri huyo ambaye kwasasa ana umri wa miaka 34 akiwa ni mwanzilishi wa taasisi iitwayo ‘Life Without Limbs’ iliyopo katika mji wa Los Angeles na amekuwa mhamasishaji maarufu na msemaji mwenye nguvu zaidi duniani akitoa masomo mbalimbali yanayohusu matumaini kwa wale waliozaliwa na ulemavu.

Ingawa amekuwa maarufu ulimwenguni kote kwa ujumbe wake unaohamasisha imani, sasa amejipanga kueneza matumaini zaidi kupitia albamu yake ya kwanza ya muziki.

Mhubiri Nick Vujicic.

“Ninafanya albamu!” Vujicic aliwatangazia wafuasi wake zaidi ya milioni 9 kupitia ukurasa wake wa Facebook katika ujumbe wa Alhamisi ya wiki iliyopita.

“Imekuwa ni ndoto yangu kwa muda mrefu sasa kuwa na uwezo wa kubeba maono ya kutangaza tumaini, kusudi na kuhamasisha watu ulimwenguni, na kuliunganisha hilo kusudi na mapenzi yangu kwenye muziki na nyimbo, na sasa hatimaye ninafanya hivyo ! ”

Kwa mujibu wa Christian Post, album hiyo itaitwa Brighter World, na inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 28 Januari 2018, ingawa tayari imeanza kununuliwa kupitia tovuti yake tovuti rasmi kabla ya uzinduzi huo rasmi mwakani.

“Siwezi kusubiri kuwatumia watu video, taarifa na picha mbalimbali ya safari ndefu niliyotoka mpaka hapa nilipo. Nasema asante kwa upendo wako, faraja na msaada,” Vujicic aliongeza.


Mhubiri Nick Vujicic akiwa na mtoto wake wa kiume.

Mhubiri huyo alielezea kwamba albamu hiyo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zenye kuinua mioyo ya watu, zenye mguso chanya na nyimbo chache zenye mguso wa imani pia kutakuwa na baadhi ya nyimbo ambazo zimegusa na kubadilisha maisha yake, na pia atatoa idadi ya nyimbo zake mpya ambazo zimeandikwa na waandishi wengine, ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe.

Mpaka sasa mhubiri Vujicic ametembelea nchi zaidi ya 58 duniania na amezungumza katika mikutano mingi ya shule na vyuo mbalimbali, matamasha ya gerezani, mikutano na maonyesho ya majadiliano duniani kote, akishuhudia watu jinsi imani yake ilivyomsaidia kupita katika kipindi cha giza ambapo hakujua ni jinsi gani angeweza kuendelea.


Mhubiri Nick Vujicic akiwa kwenye moja ya mikutano mikubwa ya wanafunzi.

Pia ameandika vitabu kadhaa, kama vile Unstoppable: The Incredible Power of Faith in Action ambacho kilitoka mwaka 2012.

Mhubiri Vujicic, kwasasa ameoa na ana watoto wawili, na mwezi juni mwaka huu aliitangazia uma kuwa mkewe, anayefahamika kwa jina la Kanae, anatarajia kupata watoto mapacha.



“Hotuba zangu kwa umma zimebeba ujumbe usiokuwa wa kidini, ila hotuba hizo zinakuwa zinalingana na imani yangu katika Yesu Kristo.



“Napenda kuwaambia watu wasikate tamaa. Wakati mwingine tunasubiri sana ili miujiza iweze kutokea katika maisha yetu na miujiza hiyo haitokei. Naaamini mambo mengi yalikuwa tofauti sana katika maisha yangu. Lakini kujua kwamba ninaweza kuwa muujiza kwa mtu mwingine hufanya maisha yangu yawe na thamani kubwa ya kuishi. “Vujicic aliuambia mtandao wa Today.com hivi karibuni.

Comments