MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

VIDEO: SAID MRISHO ALIYETOBOLEWA MACHO AFUNGUKA SAKATA LA KUITELEKEZA FAMILIA


Said Mrisho


SINEMA linaendelea. Ikiwa ni siku moja tu Bi. Stara Soud, mke wa kijana alinayedaiwa kutobolewa macho na mtu mmoja anayetajwa kwa jina la Saluma Njwete ‘Scorpion’, Said Mrisho, kuibuka na madai mazito ya kutelekezwa na mumewe, kijana huyo ametolea ufafanuzi madai hayo, ambapo amefunguka mambo mengi nyuma ya pazia.

Katika mahojiano mubashara na Global TV Online, nyumbani kwake Tabata Kisukulu, Said amesema madai mengi yaliyosemwa na Stara ni ya uongo yenye lengo la kumchafua kwa jamii ili aonekane mwenye matatizo na hafai, jambo ambalo analipinga kwa hisia kali.

“Mengi aliyosema Stara niu uongo, yeye anachotaka ni mali ambazo nimesaidiwa wakati wa matatizo yangu, anataka zile bajaji na pikipiki, ambazo niko tayari kumkabidhi mbele ya ushahidi maalum, mbona mimi nimemvumilia mambo mengi ya aibu ambayo siwezi kuyasema sana kwa sababu za kiheshima, mwanamke alikuwa anatumia simu yangu kuongea na bwana zake.

Bi. Stara Soud na watoto wake.


“Wakati mwingine natukanwa na wanaume kisa yeye tena kuna kipindi alikuwa anatoroka na kwenda klabu kulewa pombe, akiwa na mimba, kwa sasa nimeoa na mwanamke huyu ni wa zamani na yeye anamfahamu, tofauti ni kwamba huyu wa sasa ambaye jina lake ni Mariam anaangali utu lakini huyu Stara anaangalia vitu,”alisema Said na kuongeza;

“Hadi sasa tunavyoongea hapa nimeambia anahamisha tena vitu kule nilikompangishia ili aende mahali kusikojulikana, ni huyohuyo ambaye ameniletea barua kwua naitwa ustawi wa jamii siku ya Jumatatu, sijui kwa kweli amenisingizia mambo mengi sana, mara mimi ni mlevi, kitu ambacho si kweli hata kidogo, mlevi ni yeye na mimi siko tayari kabisa kuwaacha wanangu, wale ambao wana umri wa kuishi na mimi kama baba, lazima niwachukue na hao ambao kisheria napaswa kuishi nao, mimi nitawahudumia, lakini nimeumia kwa jinsi alivyonidhalilisha kwa jamii, lakini namuachia Mungu,” alisema Said kwa masikitiko zaidi.0