RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

06.07.2017: WATU WKIMSIFU MUNGU KATIKA IBADA YA KUKATA RUFAA ILIYOFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Ilikuwa ni siku ya baraka kwa watu waliofika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kushiriki ibada ya KUKATA RUFAA iliyofanyika siku ya Jumapili 06.08.2017. Katika ibada hii tulimuona Mungu akituhudumia kwa viwango vingine kupitia kipindi mbalimba na hasa kipindi cha sifa. Watu waliweza kumsifu Mungu kwa njia ya nyimbo wakiongozwa na Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Kipindi hiki kiliongozwa na Roho Mtakatifu na kusababisha uwepo wa Mungu kumfikia kila aliyefika kwaajili ya kumtukuza Mungu. Kila mtu alimtukuza kwa njia yake, watu walicheza na kumsifu huyu Yesu Kristo. Unajua Mungu wetu ni Mungu wa sifa, anapenda kuona watoto wake wakimsifu na kumuimbia. Kwa kutambua hilo Mlima wa Moto Mikocheni imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kabla ya ibada kuu kuanza wanatangulia kumsifu Mungu kwanza.


Baada ya kipindi cha sifa watu waliweza kuingia katika kipindi cha kuabudu ambapo watu waliweza kumuabudu Mungu kwa njia ya nyimbo za kuabudu. Kipindi hiki kiliongozwa na mtumishi wa Mungu Martha Komanya akiongozwa na Roho Mtakatifu.. Watu waliguswa na uwepo wa Mungu uliotanda katika nyumba ya BWANA, na wengi wao walianza kutokwa na roho chafu huku wakipiga kelele, hii inaonyesha ni jinsi gani Mungu alikuwa akishughulika na maisha ya watu.


Tuna kila sababu ya kumshukuru jinsi anavyowatumia watumishi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakiongozwa na Mh. Bishop Dr. Gertrude. Mungu amekuwa mwema sana kwani kuna baadhi ya watu wanashuhudia jinsi Mungu anavyowatendea kupitia vipindi vya sifa, kipindi cha maombezi na kipindi maalum cha maombi na maombezi.


Yawezekana unapitia changamoto katika maisha yako, ninakuomba ufike katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ukutane na nguvu za Mungu. Watu wengi wamefika mahali hapa wakiwa wamechoka kabisa lakini walipokutana na mkono wa Mungu waliweza kuinuka tena, na sasa wanafurahia ukuu wa Mungu. Mungu anakupenda sana, anatamani kukuona ukimtumikia ili aingilie kati maisha yako. 


Ibada zetu zianaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kutoka katika kituo cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. baada ya ibada utarudishwa kituo.. Mungu akubariki sana...

Martha Komanya























Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare






 























Comments