RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

06.08.2017: MCH. MADOSHI AKONGA MIOYO YA WATU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuweza kutupa Neno lake la uzima katika ibada ya Jumapili 06.08.2017 kupitia mtumishi wake Mch. Madoshi kutoka Shinyanga. Ibada hii ilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ikiwa ni kwaajili ya KUKATA RUFAA na iliyoongozwa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Tulibarikiwa sana na ujumbe kutoka Mch. Madoshi ambao tunauandaa kwa sasa kwaajili yako. Ujumbe huu utainua imani yako na kukuwezesha kuwa karibu sana na Mungu, kwahiyo endelea kufuatilia post zetu.

Pia tungependa kukualika katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. siku hii itakuwa ni siku yako ya kufunguliwa kutoka katika majaribu unayopitia. Yawezekana umehanhagika sana na hujaona mpenyo wa majibu yako, nataka kukuhakikishia kuwa Mungu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" atakwenda kuondoa mateso yako. Njoo kanisani ukiwa na imani ya kupona kwa maana yule Yesu mtenda miujiza yupo mahali hapa. Wengi walikuja na nyuso za kukata tamaa lakini baada ya kukutana na nguvu za Mungu, walitoka wakiwa na nyuso za furaha, mambo yao yamewanyookea na wanafurahia ukuu wa Mungu.

Mungu anamtumia mtumishi wake Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa njia ya tofauti sana. Watu wanapokea miujiza yao, wanapoa, wanapata safari za nje, wanaokolewa, wanafunguliwa, wanapata wake na waume wakuishi nao katika maisha yao ya ndoa, wanaoa na kuolewa, wasiozaa wanapata watoto.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kabisa kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho aumMwenge kwenye mataa DSM barabara ya Coca Cola. baada ya ibada utarudishwa kituoni...

Mch. Madoshi kutoka Shinyanga


Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare


kutoka kulia ni Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mzee Mwakitalu, Mch. Noah Lukumay,

 Kutoka kushoto ni Mch. Madoshi, Mch. Francis Machichi na Mch. Stanley Nnko



























Comments