RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

06.08.2017: TUNAMSHUKURU MUNGU KWANI WATU WAZIDI KUOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hawa ni baadhi ya watumishi wa Mungu walioamua kuokoka katika ibada ya KUKATA RUFAA iliyofanyika siku ya Jumapili 06.08.2017 Mlima wa Moto Mikocheni "B". Wachungaji waliweza kuwaongoza sala ya toba, waliwaombea, waliwabatiza kwa maji mengi na siku ya Jumatatu na Jumanne watakuwa darasani wakijifunza masomo ya kukulia wokovu hapo kanisani.
06.08.2017: MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B": WALIOKOKA
Tunamshukuru Mungu kwa kuwaokoa watu wake baada ya kuteseka kwa muda mrefu wakimtumikishwa na shetani, lakini siku ya Jumapili Mungu aliwaokoa katika mateso hayo. Wakati maombi yakifanyika, watu wengi waliguswa na nguvu za Mungu na wengi wao wakaanza kutokwa na mapepo, majini na kuanguka chini. Tunamshukuru sana Mungu baada ya kuombewa na watumishi wa Mungu waliweza kuamka na kuwa huru.

Yawezekana na wewe unatamani kuokoka lakini unasikia sauti ikikuambia usiokoke, nakushauri, ikatae hiyo sauti na mrudie BWANA kwa maana hujui kilicho mbele yako. Unaweza ukajidanganya kuwa utaokoka kesho, na pengine hiyo kesho usiione. Amua sasa kuokoka ili uwe katika mikono salama ya Yesu Kristo.

Umekuwa ukilalamika hupati watoto, kazi, ada, kodi, nyumba, viwanja, mke/mume, unalogwa, umetupiwa mapepo, umeandamwa na magonjwa na mengine kama hayo, umesahau kuwa hayo yote yanatokana na wewe kumsahau huyu Mungu.. Amua sasa kuondokana na hizo shida kwa kuokoa, kubatizwa na kuishi maisha ya kumpendaze Mungu. 

Kuokoa tu sio tiketi ya kuonyesha kuwa wewe ni mwema ila kuokoka na kutenda yale yote yaliyo mema ambayo Mungu wetu ametuagiza kuyafanya kupitia kitabu chake kitakatifu yaani Biblia.

Pengine ungetamani kufika kanisani Jumapili hii, ibada zetu zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenya mataa barabara ya Coca Cola. Mungu akubariki sana.

Mch. Stanley Nnko



















Comments