RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

06.08.2017: WATU WAMKIMBILIA YESU, IDADI YA WANAOKOKA NA KUBATIZWA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO YAZIDI KUONGEZEKA

Ndugu yangu Mungu anakuhitaji kwa kazi yake, anatamani kukuona unajishughulisha katika mambo yake ili kuokoa maisha ya watu wengine kupitia karama yako. Kuna watu wengi sana wanatamani kuokoka ila hakuna watu wa kutosha wa kuwatia moyo na kuwapa nguvu za kuweza kuchukua maamuzi ya kuokoa. Wewe umebahatika KUOKOKA ni kwasababu ya mtu fulani alifanya kitu katika maisha yako na kisababisha wewe kutamani KUOKOKA. Naomba umuonee huruma huyu ambaye hajaokoka kwa kumsaidia ili aweze kuja kwa Yesu Kristo.


Nikupongeze wewe ambaye siku ya Jumapili 06.08.2017 uliweza kuokoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", ukaongozwa sala ya toba, ukaombewa, ukabatizwa na hatimaye kumpokea Roho Mtakatifu. Uamuzi uliofanya ni sahihi kabisa, na utaona mkono wa Mungu unavyofanya kazi katika maisha yako ya wokovu. 


Mungu ataingilia katika kazi yako, familia yako, biashara yako, mipango yako, malengo yako, afya yako, masomo yako, ndoa yako, uzao wako, safari zako, kibali chako. Atazuia wabaya wako waliokuchimbia shimo. Utaishi maisha ya amani na upendo.


Wewe uliyeokoka usikose mafundisho ya kukul;ia wokovu kuanzia Jumatatu na Jumanne, utajifunza mambo mengi yatakayoinua imani yako na kumjua kiundani huyu Yesu na pia utaweza kujisimamia mwenyewe katika safari ya wokovu.


Tunakushukuru wewe uliyewatia moyo hawa ndugu zetu kwa kupitia radio, mikutano, ibada, mitandao, semina, matangazo mbalimba n.k na kusababisha watu hawa kuja kwa Yesu. Naamini Mungu wangu atafanya kitu katika maisha yako.


Ushari wangu kwako ambaye umebarikiwa kuwa na karama fulani ambayo Mungu amekupa, tumia karama yako hiyo kwa kumtangaza huyu Yesu Kristo. 


Pengine ungetamani kuokoka, nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho hapa DSM au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada utarudishwa kituoni. Mungu akubariki sana


UKISOMA TUNAOMBA U-SHARE.
















































































Comments