MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

06.08.2017: WATU WATOKWA NA MAPEPO KATIKA IBADA YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tuna kila sababu ya kusema "Asante Yesu" kwa matendo makuu anayofanya katika kanisa lake la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tulimuona Mungu akiwaponya na kuwainua watu katika kipindi cha maombi na maombezi. Kipindi hiki kiilifanyika siku ya Jumapili 06.08.2017 ambapo Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay na jopo la wachungaji walipowasha moto usiozimika wa maombi. Watu wengi walitokwa na mapepo na kuwekwa huru. Yesu kwa huruma zake aliweza kuingilia kati maisha ya watu na kuwaokoa katika mateso ya muda mrefu. Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" hajawahi kushindwa, ana nguvu za ajabu sana, anawapenda watu wote bila ya kuchagua dini, kabila, rangi au taifa.

Jamani yupo Mungu katika kanisa hili, kwani tunashuhudia watu wakifunguliwa na kuwekwa huru kupitia vinywa vya watumishi wa Mungu ambavyo vinanena mema kutoka kwa Mungu. Mungu anawatumia kwa njia ya tofauti sana na tunashuhudia kwa macho yetu kupitia shuhuda za watu.

Yawezekana unapitia magumu katika famili yako, kazi yako, ndoa yako, afya yako n.k na umehangaika bila kupata majibu, leo nataka nikupe njia sahihi ya kuondokana na mateso yako. Yupo Yesu Kristo muweza wa yote, unachotakiwa kufanya ni kuwa karibu naye, maagizo yako anayokueleza katika Biblia, kuyaisha mafundisho yako, kuungama dhambi zako, kuwapenda watu wote, kuwa na imani, uwe mtoaji kanisani kusapoti huduma yake na kutenda yale yote mema.


Tunakukaribisha katika ibada ya ya Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana

0